Meli
mbilii za Uvuvi katika bahari kuu Tao
Hang 1 na Tao Hang 7 zimetia nanga katika bandari ya Zanzibar kwa mara ya kwanza kwa Madhumuni ya kukaguliwa na
kushusha shehena ya samaki ambao hawawahitaji (Bycatch).
Meli
hizi mbili baada ya kuwasili wataalam wa Uvuvi kutoka mamlaka ya Uvuvi katika
bahari kuu walienda kuikagua iwapo inakidhi vigezo vya Uvuvi katika bahari kuu
na kuzipatia leseni ya Uvuvi hapa kwetu.
Baada
ya ukaguzi meli hizi zilionekana kukidhi matwakwa yaliyokuwa yanahitajika na
zilipewa leseni ya kuvua katika bahari kuu. Aidha samaki ambao walivuliwa kwa
bahati mbaya na ambao wao hawawahitaji walishushwa na kuuzwa kwa wananchi mjini
Zanzibar.
Mojawapo
la sharti ya kupewa leseni ni kuleta samaki hao na kuwauzia wananchi katika
nchi husika
Hivi
karibuni serikali ilisimamisha utoaji wa leseni hizi na kuzifanyia maboresho ili serikali iweze
kufaidika zaidi kutokana na Uvuvi katika bahari kuu. Maboresho hayo yamefanyika
na utoaji leseni umeanza kama ilivyopangwa
Moja kati ya meli za Uvuvi Tai Hong No 1 ikionekana kwa karibu ikiwa imetia nanga |
Mkaguzi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Uvuvi katika Bahari Kuu Bw. Zouwa akisalimiana na Captain wa meli hiyo baada ya kuingia ndani ya meli |
Moja kati ya mitego ya kuvulia samaki zinazoitwa radio boya zikikaguliwa |
Mkaguzi akiendelea kukagua floating boya zinazotumika katika kuvua samaki |
Chumba cha kuhifadhia samaki (cold room area temperature minus 60) |
Mitego ya kukamatia samaki |
Mashine mbalimbali zinazosaidia kusukuma meli |
Wafanyakazi wa meli hiyo wakifungua sehemu ya kuhifadhia samaki ili wakaguzi waweze kuona samaki waliopo |
Mmoja kati ya wamiliki wa meli hiyo ya TAI HONG akizungumza na waandishi wa habari akishukuru kwa kuwa na taratibu hizo na kuipongeza serikali kwa hatua nzuri |
Muonekano wa meli ya TAI HONG NO 1 ikiwa imetia nanga |
iko vizuri rasilimali hizi zinatakiwa kunufaisha nchi na watu wake
JibuFuta