MAAFISA UGANI WA SINGIDA NA DODOMA WAPATIWA MAFUNZO REJEA KUHUSU UFUGAJI WENYE TIJA.
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetoa mafunzo rejea kwa maafisa ugani kutoka mikoa ya Singida na Dodoma ili kuwawezesha wagani hao kwenda kutoa elimu kwa wafugaji. Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani, Dkt. Angello Mwilawa amesema wizara imekua ikitekeleza mikakati muhimu katika sekta ya mifugo ili kuweza kumsaidia mfugaji kufuga kisasa na kibiashara. Mikakati hiyo ni pamoja na Uboreshaji wa Koosafu za mifugo nchini, Udhibiti wa magonjwa, Upatikanaji wa uhakika wa malisho na maji katika maeneo yaliyo na mifugo, Kuboresha uzalishaji ulio wa kibiashara na ustawishaji wa ndege wafugwao, Kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa migogoro ya ardhi, Kuhamasisha na kuanzisha vyama vya ushirika vya wafugaji na Kudhibiti upotevu wa mapato yatokanayo na mifugo pamoja na mazao yake. Dkt. Mwilawa amesema katika kutekeleza mikakati hiyo wizara imekua ikipata changamoto nyingi ambazo ni uk...