UCHUMI WA BULUU NI FURSA - MHE. KAMANI

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ng’wasi Kamani amesema kuwa mbali na Uchumi wa buluu kuhakikisha usalama wa chakula na lishe pia ni eneo lenye fursa kubwa za ajira, uwekezaji, biashara, utalii na burudani.

Mhe. Kamani amesema hayo aliposhiriki Kongamano kubwa la uchumi wa buluu lililofanyika Agosti 12,2026 eneo la Kizimkazi lililopo Kusini Unguja visiwani Zanzibar.

Hata hivyo Mhe. Kamani amebainisha kuwa uwezo wa kunufaika na fursa hizo unategemea kwa kiasi kikubwa matumizi endelevu ya bahari na rasilimali zake ikiwa ni pamoja na maziwa, mito, mabwawa na vyanzo vingine vya maji.

“Kauli mbiu yetu ya Hifadhi Bahari, Changamkia fursa za uchumi wa Buluu ni wito wa kuchukua hatua za kuimarisha usimamizi endelevu wa rasilimali za bahari, kukabiliana na uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira pamoja na kuongeza ushiriki wa jamii katika uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali hizo” Ameongeza Mhe. Kamani.

Aidha Mhe. Kamano ameelezea umuhimu wa kutumia teknolojia, utafiti na ubunifu katika kuongeza mchango wa sekta ya Uvuvi kupitia uzalishaji wenye tija, kuongeza thamani na kuboresha ushindani wa mazao ya Uvuvi.

Kongamano hilo limefanyika ikiwa ni sehemu ya Tamasha kubwa la Kizimkazi ambalo linafanyika Visiwani Zanzibar kuanzia Agosti 12-14,2026.











Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

UTEKELEZAJI WA UFUGAJI SAMAKI KWA VIZIMBA WAANZA ZIWA TANGANYIKA

TANZANIA DAIRY BOARD