TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA 10 WA WATAALAM WA MIFUGO AFRIKA 2029
Nchi ya Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 10 wa Wataalam wa Mifugo Barani Afrika unaotarajiwa kufanyika mwaka 2029.
Uamuzi huo umefikiwa Agosti 12,2026 wakati wa Mkutano wa 9 wa Wanachama wa Jumiya ya Wataalam wa Mifugo Barani Afrika (AASAP) unaoendelea mjini Wusa, Abuja, Nigeria Kuanzia Agosti 9 hadi 13 2026 ambapo wataalam hao wamekubaliana na kufikia uamuzi huo baada ya kuvutiwa na jitihada za Tanzania kwenye upande wa maendeleo ya Sekta ya Mifugo.
Awali kabla ya uamuzi huo Mwakilishi wa Tanzania katika Mkutano huo, Dkt. Titus Lyatuu ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Wataalam wa Mifugo Tanzania (TSAP) alieleza utayari wa Tanzania katika maandalizi na uendeshaji wa Mkutano huo huku akibainisha fursa nyingi mbalimbali za tafiti na maendeleo zilizopo nchini.
Dkt. Lyatuu alieleza pia vivutio vilivyoko nchini Tanzania kwa upande wa sekta ya Utalii, tamaduni za watu wa Tanzania, hali ya amani na usalama iliyopo nchini na mifumo ya ufugaji inayoendelea kuboreshwa chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Chama cha Wataalam wa Mifugo Tanzania (TSAP) kinatarajia kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya Mifugo ili kufanikisha Mkutano huo mkubwa wa wataalam wa Mifugo.

Maoni
Chapisha Maoni