SERIKALI KUONGEZA UWEKEZAJI KATIKA MIUNDOMBINU YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwekeza katika uboreshaji wa miundombinu ya elimu na mafunzo ya ufundi ustadi ili kuendelea kujenga  taifa la kujitegemea kupitia elimu ya amali.

Amesema hayo Wakati wa ziara yake mkoani Mara leo Agosti 12, 2026 baada Kukagua na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Amali na Ufundi Musuguri iliyopo Wilayani Butiama inayogharimu shilingi bilioni 1.6. 

" Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwekeza katika uboreshaji wa  miundombinu ya elimu na mafunzo ya amali ili kutengeneza taifa linaloweza kujitegemea kupitia vijana kama alivyoasisi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, hivyo ujenzi wa shule za amali kama hii ya Musuguri utatusaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini" alisema Dkt. Bashiru.

Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Butiama amewataka wananchi hao kuwa wa mfano katika kuilinda na  kuitetea misingi iliyoachwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwa ni pamoja kuendeleza elimu ya mafunzo na kujitegemea.

Aidha, katika hatua nyingine, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ametoa rai kwa wananchi, wanasiasa, watendaji wa umma pamoja na sekta binafsi kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kutekeleza kwa vitendo Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Akiwa Wilayani Butiama Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amezindua Nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Butiama.

Baada ya kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya Wilaya ya Butiama, msafara wake unaekelea Wilayani Bunda kwa ajili ya kukagua na kuzindua miradi pamoja kuongea na wananchi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa alipokuwa akizungumza baada ya Kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Shule ya Secondari ya Elimu ya Amali Musuguri iliyopo Butiama, Wakati wa Ziara yake Wilayani humo Agosti 12, 2026.

Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi na Amali Musuguri iliyopo Wilayani Butiama, mkoa Mara ambaye ujenzi wake umefikia asilimia 90% huku gharama za mradi huo ni shilingi Bilioni 1.6.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akifurahia baada ya kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi na Amali Musuguri leo Agosti 12, 2026 Wilayani Butiama Mkoa wa Mara.

Baadhi ya wanafunzi wanaosoma Shule ya Sekondari ya Amali na Ufundi Musuguri iliyopo Butiama mkoani Mara, wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi wakati wa ziara yake shuleni hapo .

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

UTEKELEZAJI WA UFUGAJI SAMAKI KWA VIZIMBA WAANZA ZIWA TANGANYIKA

TANZANIA DAIRY BOARD