KATIBU MKUU MEENA AFUNGUA KIKAO CHA KUJADILI FURSA ZA UWEKEZAJI KUPITIA SGR

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agness Meena, amefungua kikao cha kujadili fursa za uwekezaji wa kiuchumi kupitia Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), kikao kilichofanyika Agosti 10, 2026, Mtumba jijini Dodoma.

Kikao hicho kililenga kujadili na kubainisha fursa mbalimbali za kiuchumi zinazoweza kunufaisha sekta ya mifugo na uvuvi pamoja na kilimo kupitia uwepo na maendeleo ya miundombinu ya SGR, sambamba na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa maendeleo katika kukuza uwekezaji nchini.

Kikao hicho kilishirikisha wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na taasisi zake, wataalam kutoka Wizara ya Kilimo, pamoja na wawakilishi kutoka Benki ya Dunia, ambao walishiriki katika kubadilishana uzoefu na kutoa mapendekezo kuhusu namna bora ya kutumia fursa zinazotokana na mradi huo kwa ajili ya kukuza shughuli za kiuchumi.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

UTEKELEZAJI WA UFUGAJI SAMAKI KWA VIZIMBA WAANZA ZIWA TANGANYIKA

TANZANIA DAIRY BOARD