DKT. MWIGULU AHIMIZA UFUGAJI WA KISASA KUONGEZA UZALISHAJI NA TIJA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amewahimiza wataalam na wadau sekta ya mifugo nchini kuendelea kutoa  mafunzo ya ufugaji bora na wa kisasa  kwa wananchi wote ili kuwa na tija katika uzalishaji katika sekta ya mifugo.

Mhe. Dkt. Nchemba amesema hayo mara baada ya kukagua shughuli za ufugaji  katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki leo Agosti 04, 2026 ambapo kwa kanda hiyo maonesho hayo yanafanyika Mkoani Morogoro.

Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Nchemba alivutiwa na ng'ombe aliyefugwa na Magereza ya mkoani Morogoro ambaye anauwezo wa  kuzalisha Lita 30 za maziwa kwa siku na kuielekeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na taasisi hiyo kuendelea kutoa elimu ya uzalishaji wenye tija kwa wananchi kupitia mafunzo na ugani.

Aidha, Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Nchemba alisema ili kukabiliana na changamoto za uhaba wa maeneo kwa ajili ya ufugaji ni muhimu wadau wa sekta ya mifugo kujifunza mbinu za ufugaji wa kisasa wenye tija na utakaoendana na mahitaji ya soko kwa kuzingatia upatikanaji wa maeneo kwa ajili ya shughuli hiyo.

Kwa Upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema kuwa sekta za uzalishaji ikiwemo kilimo, mifugo na uvuvi zinahitaji tafiti, ubunifu na teknolojia nzuri ili kuongeza uzalishaji utakaochochea magauzi ya kiuchumi nchini.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akimfafanulia Jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba katika Banda la Maonesho ya Nane Nane la Magereza ya Morogoro leo Agosti 4, 2026.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (wa kwanza kulia) akizungumza na Watendaji na Watumishi wa Magereza Mkoani Morogoro (hawapo pichani) baada ya kutembelea na kukagua miradi yao ya ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na nyama katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki leo Agosti 4, 2026 mkoani Morogoro.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akimuonesha Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba malisho ya mifugo katika Banda la Maonesho la Magereza mkoani Morogoro leo Agosti 04, 2026.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akipata maelezo ya kutoka kwa mfugaji anayemiliki ng'ombe mwenye Kilogramu 1,050 mwenye thamani ya shilingi Milioni 20 Baada Kumtembelea mfugaji huyo katika maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki leo Agosti 4, 2026

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba(watatu kulia) akifanya majumuisho ya ziara yake katika maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki 2026 iliyofanyika leo Agosti 4, 2026 mkoani Morogoro.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

UTEKELEZAJI WA UFUGAJI SAMAKI KWA VIZIMBA WAANZA ZIWA TANGANYIKA

TANZANIA DAIRY BOARD