DKT. BASHIRU: SERIKALI ITASHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KUTATUA CHANGAMOTO ZA TASNIA YA KUKU

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi  Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema kuna haja ya serikali kushirikiana na sekta binafsi katika kusimamia ubora wa uzalishaji wa vifaranga vya kuku, chanjo pamoja na chakula cha kuku ili tasnia hiyo iweze kuendelea kukua na kuchangia uchumi na usalama wa chakula.

Mhe.Balozi Dkt. Bashiru ameeleza hayo Agosti 10, 2026  baada kufika katika shamba la uzalishaji wa kuku la Homeland Farm lililopo Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza ambapo amesema ushirikiano wa serikali na sekta binafsi utajikita zaidi katika udhibiti wa mifumo ya kulinda ubora wa tasnia ya kuku hususan uzalishaji wa vifaranga vyenye ubora, chakula cha kuku na chanjo.

"Yale ambayo sekta binafsi inauwezo nayo tushirikiane nayo, yale ambayo serikali tunapaswa kufanya mfano ya udhibiti, mfano haiwezekani mtu yuko sokoni anauza vifaranga viko chini ya ubora" alisema Mhe. Balozi Dkt. Bashiru.

Aidha, alisema kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo zimepanga kuwa na ushirikiano kupitia mkakati wa kuzalisha Soya ambayo inatumika kwa kiwango kikubwa katika uzalishaji wa chakula cha samaki ili kupunguza uagizaji wa soya kutoka nje ya nchi ambayo imekuwa ikisababisha kuongezeka kwa gharama za vyakula vya kuku na samaki.

Kwa Upande Wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shamba la Ufugaji Kuku wa Nyama na Mayai Homeland Farm Bi. Mwanabure Ihuya amesema shamba lina idadi ya kuku 60,000 wa nyama na mayai ambapo uzalishaji wake kwa sasa ni trei 850 za mayai kwa siku na tani 28 za nyama kwa mwezi huku likiajiri zaidi watu 150 kwa ajira za kidumu na muda.

Aidha, Bi. Ihuya alieleza baadhi ya changamoto ikiwemo gharama kubwa za uzalishaji hususan bei ya vifaranga, madawa, vyakula vya kuku, uwepo wa vifaranga visivyokuwa na ubora, ambapo Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akazitolea ufufanuzi na kutoa msimamo wa serikali katika kutatua changamoto hizo.








Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

UTEKELEZAJI WA UFUGAJI SAMAKI KWA VIZIMBA WAANZA ZIWA TANGANYIKA

TANZANIA DAIRY BOARD