DKT. BASHIRU AKAGUA NA KUZINDUA MIRADI YA MAENDELEO MKOANI MARA
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amekagua na kuzindua miradi ya mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali mkoani Mara na kueleza kuwa serikali itaendelea kutoa kipaumbele katika kutenga fedha kwa wakati katika ujenzi na uboreshaji miundombinu ya barabara, umeme na maji ili miradi hiyo ikamalishwe kwa wakati.
Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesema hayo leo Agosti 11, 2026 wakati wa ziara yake maalum ya siku nne inayolenga kutembelea, kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali mkoani Mara.
Katika ziara hiyo Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amezindua Daraja la Majengo mapya - Pambazuko lenye thaman ya zaidi ya shilingi milioni 287 ambalo litaunganisha Kata za Bweri na Rwamlimi ndani ya Manispaa ya Musoma.
Pia, alitembelea na kukagua ujenzi wa Soko la Nyayo, Kituo cha Mabasi na Barabara za mitaa ndani ya Manispaa ya Musoma, kuweka jiwe la Msingi la Madarasa matano, matundu ya vyoo na Ofisi katika shule ya Msingi Jitirola na kukagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kiriba iliyojengwa kwa nguvu za wananchi na serikali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
Kwa Upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Kanali Evans Mtambi amesema mradi wa ujenzi wa soko, Kituo cha Mabasi na Barabara za Mitaa ndani ya Manispaa ya Musoma utafungua fursa ya uwekezaji na uzalishaji kiuchumi ambapo jumla ya gharama za mradi huo ni shilingi biloni 19.6.
Ziara hiyo ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa mkoani Mara inatarajiwa kuendelea hapo kesho Agosti 12, 2026 katika Wilaya ya Butiama na Bunda.






Maoni
Chapisha Maoni