CAG AVUTIWA NA MIKAKATI YA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI KUIMARISHA UVUVI WA BAHARI KUU


Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Charles Kichere ametembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Kitaifa ya nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni Dodoma ambapo alipata fursa ya kujionea mafanikio na mikakati mbalimbali ya Serikali katika kuendeleza sekta ya uvuvi hususan uvuvi wa bahari kuu, ziara hiyo imefanyika leo tarehe 07 Agosti 2026.

Akiwa katika banda hilo CAG alipokea maelezo kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) Dkt. Mathew Silas kuhusu mikakati ya Wizara ya kuongeza tija na mchango wa sekta ya uvuvi katika uchumi wa taifa Dkt. Silas alieleza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha sekta ya uvuvi inachangia kufikia lengo la asilimia 10 katika uchumi kupitia uwekezaji, usimamizi endelevu wa rasilimali za uvuvi wa bahari kuu na uimarishaji wa miundombinu ya sekta hiyo.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

UTEKELEZAJI WA UFUGAJI SAMAKI KWA VIZIMBA WAANZA ZIWA TANGANYIKA

TANZANIA DAIRY BOARD