WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI MBIONI KUANZISHA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA

Wizara ya Mifugo na Uvuvi ipo katika hatua za mwisho za kuanzisha Kituo cha Huduma kwa Wateja kitakacholenga kupokea, kusikiliza na kushughulikia changamoto za wadau wa sekta ya mifugo na uvuvi, sambamba na kutoa taarifa na ufafanuzi kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi kuhusu utoaji wa huduma bora kwa wateja yaliyofanyika leo, Julai 8, 2026, jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Mhina, amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za wizara kuboresha utoaji wa huduma kwa wafugaji, wavuvi na wadau wengine wa sekta hizo.

Dkt. Mhina amesema mafunzo hayo yanawahusisha wataalamu walioteuliwa kutoka idara na vitengo mbalimbali vya wizara, kwa lengo la kuwajengea uwezo na ujuzi katika utoaji wa huduma bora kwa wateja, ambao utakuwa msingi wa ufanisi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja.

"Mafunzo haya yamejumuisha wataalamu walioteuliwa kutoka idara na vitengo mbalimbali vya wizara, lengo kuu ni kuwajengea uwezo watumishi hao kwa kuwapatia mafunzo ya utoaji wa huduma bora kwa wateja," amesema Dkt. Mhina.

Ameongeza kuwa timu hiyo haitajikita katika utoaji wa huduma kwa wateja pekee, bali pia itashiriki kushughulikia masuala mbalimbali yatakayochochea mageuzi ya kiutendaji ndani ya wizara na kuongeza tija katika sekta za mifugo na uvuvi, hatua itakayowanufaisha wafugaji, wavuvi na wadau wengine kwa kuongeza uzalishaji na kuboresha huduma.

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Mhina, akielezea na kufafanua lengo la Mafunzo ya Huduma kwa Wateja kwa Watumishi wa Wizara hiyo, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara hiyo kuhusu utoaji wa huduma bora kwa wateja, Mafunzo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo - Mtumba, Julai 8, 2026 Dodoma.

Afisa Tawala Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Wamoja Ayubu, akitoa neno la Utangulizi, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara hiyo kuhusu utoaji wa huduma bora kwa wateja, Mafunzo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo - Mtumba, Julai 8, 2026 Dodoma.

Mhadhiri Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) - Dodoma, Bw. Julius Tarimo, akielezea maana ya Huduma kwa Wateja na Sifa za Mhudumu Bora kwa Wateja, wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhusu utoaji wa huduma bora kwa wateja, Mafunzo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo - Mtumba, Julai 8, 2026 Dodoma.

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakiwa katika mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu utoaji wa huduma bora kwa wateja, Mafunzo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo - Mtumba, Julai 8, 2026 Dodoma.





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UTEKELEZAJI WA UFUGAJI SAMAKI KWA VIZIMBA WAANZA ZIWA TANGANYIKA

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI