TANZANIA YAPATA HESHIMA KUWA MWENYEJI KUANDAA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UKUZAJI VIUMBEMAJI

Na. Stanley Brayton

◾Dkt. Bashiru azindua Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uvuvi Tanzani (TAFICO) na Kitabu cha Mapishi ya Samaki.

Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la Ukuzaji Viumbemaji Duniani (WA26T) na Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Afrika (AFRAQ26), baada ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jumuiya ya Wakuzaji Viumbemaji Duniani (WAS) kusaini hati ya makubaliano ya maandalizi ya kongamano hilo litakalofanyika nchini Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), kuanzia Desemba 1 hadi 4, 2026.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo Julai 13, 2026 Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, kwa niaba ya Serikali, huku WAS ikiwakilishwa na Mwenyekiti wa Tawi la Afrika (AFRAQ), Prof. Julius Manyala.

Akizungumza baada ya utiaji saini huo, Mheshimiwa Balozi Dkt. Bashiru alisema uteuzi wa Tanzania kuwa mwenyeji wa kongamano hilo ni matokeo ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta ya ukuzaji viumbemaji, hususan ongezeko la uzalishaji kwa zaidi ya asilimia 300 ndani ya kipindi cha miaka mitano.

Alifafanua kuwa uzalishaji wa viumbemaji umeongezeka kutoka tani 44,700 katika mwaka wa fedha 2020/2021 hadi tani 181,535.76 mwaka 2025/2026, hatua aliyoeleza kuwa imechangiwa na sera za Serikali za kuboresha mazingira ya uwekezaji, kuimarisha tafiti, kuendeleza matumizi ya teknolojia na kuongeza ushiriki wa sekta binafsi.

"WAS imeionesha Tanzania imani kubwa kwa kuipa fursa ya kuwa mwenyeji wa kongamano hili, na hii ni nafasi muhimu ya kuitangaza nchi yetu na kuonesha mafanikio tuliyoyapata katika sekta ya ukuzaji viumbemaji na Uchumi wa Buluu," alisema.

Alisema kongamano hilo linatarajiwa kushirikisha zaidi ya wajumbe 2,000 kutoka zaidi ya mataifa 100, wakiwemo watafiti, wawekezaji, watunga sera, wabunifu wa teknolojia na washirika wa maendeleo.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, mkutano huo utafungua fursa za kuvutia uwekezaji, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kubadilishana teknolojia na kuongeza masoko ya bidhaa za sekta ya uvuvi na ukuzaji viumbemaji.

Aliwataka wadau wote, wakiwemo vyuo vikuu, taasisi za utafiti, sekta binafsi, taasisi za fedha na mamlaka za serikali za mitaa, kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya kongamano hilo ili kuhakikisha linafanikiwa na kuleta manufaa kwa taifa.

Katika hafla hiyo, Mheshimiwa Balozi Dkt. Bashiru pia alizindua Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), yenye wajumbe wanane, pamoja na Kitabu cha Mapishi ya Samaki – Tanzania kilichoandaliwa kwa ushirikiano wa Serikali, WorldFish na Aquatic BioSolutions Tanzania (ABiST) kupitia Mradi wa PROFISHBLUE.

Alisema kitabu hicho kitasaidia kuhamasisha ulaji wa samaki, kuboresha lishe ya wananchi, kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi na ukuzaji viumbemaji, pamoja na kupanua fursa za masoko ya bidhaa za sekta hiyo.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Uvuvi), Prof. Mohamed Ali Sheikh amesema Serikali imejiandaa vizuri kwa kuhakikisha Kongamano hilo linakuwa la kihistoria hapa nchini.

Naye, Mwakilishi wa WAS, ambaye ni Mwenyekiti wa AFRAQ, Prof. Julius Manyala ameishukuru Tanzania kwa kukubali kuwa Mwenyeji na Muandaaji wa Kongamano hilo.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, akihutubia wadau wa Sekta ya Uvuvi, katika Hafla ya Uzinduzi na Utiaji Saini wa Makubaliano ya Tanzania kuwa Mwenyeji na Muandaaji wa Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Duniani kwa mwaka 2026 (WA26T) na Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Afrika (AFRAQ26) pamoja na Uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), iliyofanyika katika Ukumbi wa TAFICO - Kigamboni, Julai 13, 2026 Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Prof. Mohamed Sheikh, akizungumza na wadau wa Sekta ya Uvuvi, katika Hafla ya Uzinduzi na Utiaji Saini wa Makubaliano ya Tanzania kuwa Mwenyeji na Muandaaji wa Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Duniani kwa mwaka 2026 (WA26T) na Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Afrika (AFRAQ26) pamoja na Uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), iliyofanyika katika Ukumbi wa TAFICO - Kigamboni, Julai 13, 2026 Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji Nchini, Dkt. Nazael Madalla, akitoa neno la Utangulizi, katika Hafla ya Uzinduzi na Utiaji Saini wa Makubaliano ya Tanzania kuwa Mwenyeji na Muandaaji wa Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Duniani kwa mwaka 2026 (WA26T) na Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Afrika (AFRAQ26) pamoja na Uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), iliyofanyika katika Ukumbi wa TAFICO - Kigamboni, Julai 13, 2026 Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa AFRAQ, Prof. Julius Manyala, akitoa neno la Shukrani kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukubali kuwa Mwenyeji wa Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Duniani, katika Hafla ya Uzinduzi na Utiaji Saini wa Makubaliano ya Tanzania kuwa Mwenyeji na Muandaaji wa Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Duniani kwa mwaka 2026 (WA26T) na Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Afrika (AFRAQ26) pamoja na Uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), iliyofanyika katika Ukumbi wa TAFICO - Kigamboni, Julai 13, 2026 Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Prof. Mohamed Sheikh (kulia) na Mwenyekiti wa AFRAQ, Prof. Julius Manyala (kushoto), wakikabidhiana hati za Makubaliano ya Tanzania kukubali kuwa Mwenyeji wa Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Duniani, katika Hafla ya Uzinduzi na Utiaji Saini wa Makubaliano ya Tanzania kuwa Mwenyeji na Muandaaji wa Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Duniani kwa mwaka 2026 (WA26T) na Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Afrika (AFRAQ26) pamoja na Uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), iliyofanyika katika Ukumbi wa TAFICO - Kigamboni, Julai 13, 2026 Dar es Salaam.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (katikati), akizindua Kitabu cha Mapishi ya Samaki, katika Hafla ya Uzinduzi na Utiaji Saini wa Makubaliano ya Tanzania kuwa Mwenyeji na Muandaaji wa Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Duniani kwa mwaka 2026 (WA26T) na Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Afrika (AFRAQ26) pamoja na Uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), iliyofanyika katika Ukumbi wa TAFICO - Kigamboni, Julai 13, 2026 Dar es Salaam, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TAFICO, Prof. Yunus Mgaya.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (wa tatu kushoto), akiwa na Viongozi mbalimbali wakiwa wameshikilia Vitabu vya Mapishi ya Samaki, katika Hafla ya Uzinduzi na Utiaji Saini wa Makubaliano ya Tanzania kuwa Mwenyeji na Muandaaji wa Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Duniani kwa mwaka 2026 (WA26T) na Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Afrika (AFRAQ26) pamoja na Uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), iliyofanyika katika Ukumbi wa TAFICO - Kigamboni, Julai 13, 2026 Dar es Salaam.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (kulia), akimkabidhi nyaraka za Utendaji kazi Afisa Mtendaji Makuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), CPA Shaibu Matessa (kushoto), katika Hafla ya Uzinduzi na Utiaji Saini wa Makubaliano ya Tanzania kuwa Mwenyeji na Muandaaji wa Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Duniani kwa mwaka 2026 (WA26T) na Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Afrika (AFRAQ26) pamoja na Uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), iliyofanyika katika Ukumbi wa TAFICO - Kigamboni, Julai 13, 2026 Dar es Salaam.

Wadau wa Sekta ya Uvuvi wakiwa katika Hafla ya Uzinduzi na Utiaji Saini wa Makubaliano ya Tanzania kuwa Mwenyeji na Muandaaji wa Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Duniani kwa mwaka 2026 (WA26T) na Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Afrika (AFRAQ26) pamoja na Uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), iliyofanyika katika Ukumbi wa TAFICO - Kigamboni, Julai 13, 2026 Dar es Salaam.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (wa Sita kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Sekta ya Uvuvi, katika Hafla ya Uzinduzi na Utiaji Saini wa Makubaliano ya Tanzania kuwa Mwenyeji na Muandaaji wa Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Duniani kwa mwaka 2026 (WA26T) na Kongamano la Ukuzaji Viumbemaji Afrika (AFRAQ26) pamoja na Uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), iliyofanyika katika Ukumbi wa TAFICO - Kigamboni, Julai 13, 2026 Dar es Salaam.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UTEKELEZAJI WA UFUGAJI SAMAKI KWA VIZIMBA WAANZA ZIWA TANGANYIKA

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI