PROF. SHEIKH AKAGUA MRADI WA BBT UVUVI MWANZA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Prof. Mohammed Ali Sheikh Julai 11, 2026 amekagua maendeleo ya mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi kupitia Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT UVUVI) eneo la Nyegezi jijini Mwanza ambao ni sehemu ya shilingi bilioni 7 za mkopo zilizotolewa na serikali kwa vijana.

Akikagua mradi huo kwa niaba ya Katibu Mkuu Prof. Sheikh ameridhishwa na hatua iliyofikiwa na kueleza kuwa serikali inaendelea kuboresha sera, sheria na kanuni za uvuvi ili kuongeza uzalishaji wa samaki nchini na kuwahimiza vijana hao kupanua wigo katika kufanya ubunifu wa kuongeza thamani ya mazao hayo.

Katika hatua nyingine Prof. Sheikh amewatembelea wawekezaji wanaozalisha vifaranga vya samaki jijini Mwanza ambapo aliiagiza Idara ya Ukuzaji Viumbe maji kwa kushirikiana na  Maabara ya Taifa ya Uvuvi na Taasisi  ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania  kufanya utafiti wa vinasaba vya samaki ili kubaini ubora wa samaki wanaozalishwa na wawekezaji hao.

Naye Msimamizi wa mradi wa BBT Uvuvi ukanda wa nyegezi ambaye pia ni Kaimu Meneja wa Wakala ya  Mafunzo ya Uvuvi Tanzania (FETA) Bw. Peter Masumbuko amesema  jumla ya vijana 80 wamekuwa wakiwasimamia kufuga samaki kwenye vizimba ambao wanatarajia kuvuna tani 200 za samaki pindi watakapoanza mavuno yao mwezi Novemba Mwaka huu.

Mnufaika wa mradi wa BBT Uvuvi Bw.Shija Nchungwa ameishukuru  serikali kuwekeza kwenye mradi huo ambao umewasaidia vijana kujiajiri huku kwa upande wake binafsi akitarajia kupata takriban milioni 30 baada kuvuna samaki wake.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Prof. Mohammed Ali Sheikh (wa pili kushoto) akilisha chakula samaki kwenye moja ya Kizimba cha Mnufaika wa Mradi wa BBT Uvuvi eneo la Nyegezi Mwanza wakati wa ziara yake tarehe 12 Julai 2026

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Prof. Mohammed Ali Sheikh akiwa ameshika samaki aina sato wakati wa ziara yake jijini Mwanza tarehe 12 Julai 2026






Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Prof. Mohammed Ali Sheikh akiwa kwenye picha ya pamoja na wanufaika wa Mradi wa BBT Uvuvi eneo la Nyegezi Mwanza wakati wa ziara yake iliyofanyika Julai 12, 2026

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UTEKELEZAJI WA UFUGAJI SAMAKI KWA VIZIMBA WAANZA ZIWA TANGANYIKA

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI