WAFUGAJI WATAJWA KUWA KINARA UTEKELEZAJI DIRA YA MAENDELEO 2050
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema wizara hiyo imeanza mchakato wa kufanya mapitio ya sera ya mifugo ya mwaka 2006 na kuandaa mkakati mahususi utakaofanikisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Balozi Dkt. Bashiru amesema hayo Chalinze Mkoani Pwani kwenye Maonesho na Mnada wa Mifugo yanayofanyika katika Ranchi ya Mbogo Farm kuanzia Juni 19 hadi 22 na kueleza kuwa mikakati hiyo itasaidia kuwa na uwiano wa vipaumbele vya wizara na Dira ya Maendeleo 2050.
“Kwa mujibu wa Dira, sekta binafsi inatarajiwa kuchangia katika uchumi wa nchi kwa asilimia 70 ifikapo 2050 na wafugaji ndio sekta binafsi tangu kuzaliwa kwa ufugaji, kwahiyo wao ndio watakuwa wa kwanza kuifikia hiyo asilimia 70” amesema Balozi Dkt. Bashiru.
Aidha, ameleza kuwa Serikali imeendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuimarisha na kuendeleza sekta ya mifugo nchini akitolea mfano Mbogo Ranchi ambayo imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika uzalishaji wa mbegu na malisho na uimarishaji wa mbegu za mifugo bora.
Maonesho hayo yanendelea leo eneo la Ubena Zomozi Chalinze, Pwani kwenye Ranchi za Mbogo Farm ikiwa ni Siku ya Pili baada kuzinduliwa hapo jana na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ambapo wadau wanaendelea kujifunza teknolojia mbalimbali za ufugaji uzalishaji wa malisho na vyakula vya wanyama, mbinu za bora za ufugaji.

Maoni
Chapisha Maoni