MRADI WA BBT KUTENGENEZA AJIRA 6000 KWA WANAWAKE NA VIJANA

Na. Stanley Brayton, WMUV

Mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ya Unenepeshaji wa Mbuzi na Kilimo cha Malisho, ambao unatekelezwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, umepanga kuwawezesha wanawake na vijana 6000 ndani ya muda wake wa utekelezaji wa Miaka Mitano wa Mradi huo, ambao ukiwa na lengo la kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana katika ujasiliamali wa Biashara ya Mifugo.

Akizungumza leo Juni 1, 2026 Mkoani Morogoro, katika Warsha ya Upitiaji, Uhakiki wa Uwasilishaji wa Ripoti ya awali ya Jinsia na Ujumuishaji wa Kijamii katika Programu hiyo ya BBT, Meneja Mradi wa BBT Upande wa Jinsia na Ujumuishaji wa Kijamii, Bi. Neema Urassa amesema Mradi huo una lengo la kuwawezesha Wanawake na Vijana kupitia shughuli za unenepeshaji wa Mbuzi na Kondoo kibiashara pamoja na Kilimo cha Malisho ya Mifugo.

"Mradi huu unawalenga zaidi Wanawake na vijana, ambao kupitia Mradi huu watapata kujifunza vitu mbalimbali kwa vitendo katika mnyororo mzima wa thamani wa mazao ya mifugo, hususan mbuzi na Kondoo na Kilimo cha Malisho ya Mifugo, ili baadae wawe na uwezo wa kuingia kwenye biashara za unenepeshaji wa mifugo kwa lengo la kujiongezea kipato pamoja na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa." Amesema Bi. Urassa

Aidha, Bi. Urassa amesema baada ya vijana kupata ujuzi huo, matarajio ya Serikali ni kuwa vijana wataweza kujiajiri wenyewe, kuanzisha biashara zao, na kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto ya ajira nchini, ambapo vijana watakaonufaika watakuwa na fursa ya kupatiwa mikopo isiyo na dhamana kwa ajili ya kuendeleza biashara zao baada ya mafunzo.

Vilevile, Bi. Urassa,  ameweka wazi kuwa Mradi huo unatokana na Uongozi madhubuti wa Serikali ya Awamu ya Sita wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutambua kwa kina changamoto ya ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana, ndiyo maana Mheshimiwa Rais amechukua juhudi za makusudi kuhakikisha fedha hizo zinapatikana kwa ajili ya kuboresha maisha ya vijana kupitia miradi yenye tija kama huo wa BBT ambao unaendana na Dira ya Taifa ya Mwaka 2050.


Meneja Mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ya Unenepeshaji wa Mbuzi na Kilimo cha Malisho Upande wa Jinsia na Ujumuishaji wa Kijamii, Bi. Neema Urassa, akitoa neno la Utangulizi juu ya Mradi wa BBT, katika Warsha ya Upitiaji, Uhakiki wa Uwasilishaji wa Ripoti ya awali ya Jinsia na Ujumuishaji wa Kijamii katika Programu hiyo ya BBT, iliyofanyika katika Ukumbi wa FLOMI Hoteli, Juni 1, 2026 Morogoro.

Mtaalam wa Ufuatiliaji na Tathmini Mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ya Unenepeshaji wa Mbuzi na Kilimo cha Malisho, Bw. Tumsime Mutta, akielezea kwa ujumla Malengo ya Mradi huo wa BBT, katika Warsha ya Upitiaji, Uhakiki wa Uwasilishaji wa Ripoti ya awali ya Jinsia na Ujumuishaji wa Kijamii katika Programu hiyo ya BBT, iliyofanyika katika Ukumbi wa FLOMI Hoteli, Juni 1, 2026 Morogoro.

Mshauri elekezi wa Mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ya Unenepeshaji wa Mbuzi na Kilimo cha Malisho, Prof. Fatihia Massawe, akiwasilisha Ripoti ya Ushirikishwaji wa Kijinsia na Kijamii na Mkakati wa Jinsia katika Mradi, wakati wa Warsha ya Upitiaji, Uhakiki wa Uwasilishaji wa Ripoti ya awali ya Jinsia na Ujumuishaji wa Kijamii katika Programu hiyo ya BBT, iliyofanyika katika Ukumbi wa FLOMI Hoteli, Juni 1, 2026 Morogoro.

Picha ni Wadau mbalimbali wa Sekta ya Mifugo, wakiwa katika Warsha ya Upitiaji, Uhakiki wa Uwasilishaji wa Ripoti ya awali ya Jinsia na Ujumuishaji wa Kijamii katika Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ya Unenepeshaji wa Mbuzi na Kilimo cha Malisho, iliyofanyika katika Ukumbi wa FLOMI Hoteli, Juni 1, 2026 Morogoro.

Picha ni Wadau mbalimbali wa Sekta ya Mifugo, wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya Warsha ya Upitiaji, Uhakiki wa Uwasilishaji wa Ripoti ya awali ya Jinsia na Ujumuishaji wa Kijamii katika Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) ya Unenepeshaji wa Mbuzi na Kilimo cha Malisho, iliyofanyika katika Ukumbi wa FLOMI Hoteli, Juni 1, 2026 Morogoro.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

WAFUGAJI WAHIMIZWA KUPANDA MALISHO YA MIFUGO