JAMII YATAKIWA KUONGEZA JUHUDI MAPAMBANO DHIDI YA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI.

Wananchi wametakiwa kuongeza juhudi katika kupambana na athari zinazotokana na mabadiliko ya hali ya nchi yanayoikumba nchi na dunia kwa ujumla.

Wito huo umetolewa  leo Juni 1, 2026 na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Kwagilwa Reuben (MB) wakati akifungua maadhimisho ya wiki ya mazingira katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma.

Mhe. Kwagilwa amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha mazingira yanatunzwa ili kuwezesha nchi kutimiza mipango ya Dira 2050 kwani athari za mabadiliko ya tabia ya nchi yana athari hasi kwenye uchumi wananchi na dunia.

“Mazingira ni Uchumi pia mazingira ni afya, tunatakiwa kuyatunza  mazingira yetu ili malengo yetu ya Dira ya Taifa 2050 yanatimia.  Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi tutaendelea kutekeleza wajibu wetu  katika kulinda mazingira.” Amesisitiza Mhe.Kwagilwa.

Kwa upande wake mratibu wa maonesho hayo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Bw. Maxmilian Zitatu amesema kuwa TALIRI inazalisha na kusambaza aina 5 za mbegu za malisho  amabazo zinasaidia katika kuzuia mmomonyoko wa udongo, zinazostahimili ukamae na zinazoongeza rutuba kwenye udongo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kikundi cha Furaha Women Group na Katibu Msaidizi wa Tanzania Women Fish Workers Association (TAWFA), Bi. Fatuma Katulla ambaye ni mdau wa Maabara ya Uvuvi  amesema,  maabara ina jukumu muhimu la kufanya uchunguzi wa mabaki ya kemikali na viuatilifu kwenye mazao ya uvuvi pamoja na kutoa elimu kuhusu matumizi salama ya kemikali ili kulinda afya ya binadamu na mazingira.

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Reuben Kwagilwa akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambayo yameanza Leo Juni 1, 2026 kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma.

Mdau wa Uvuvi Bi. Fatuma Katulla ambaye ni Katibu Msaidizi wa Tanzania Women Fish Workers Association ( TAWFA) akitoa maelezo Kwa Mgeni Rasmi( hayupo pichani)  kuhusu shughuli za uvuvi Katika kutunza mazingira kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani yaliyoanza Leo Juni 1, 2026 Katika viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma

Mdau wa Uvuvi Bi. Fatuma Katulla ambaye ni Katibu Msaidizi wa Tanzania Women Fish Workers Association (TAWFA) akimkabidhi Zawadi za mazao ya Uvuvi Mgeni Rasmi ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Reuben Kwagilwa kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani yaliyoanza Leo Juni 1, 2026 Katika viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma


Mratibu wa Maonesho kutoka Taasisi ya Utafiti na Mifugo Tanzania (TALIRI), Bwa. Maximilian Zitatu akitoa maelezo Kwa Mgeni Rasmi kuhusu shughuli zinazofanywa na Taasisi hiyo Katika kutunza mazingira kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani Leo Juni 1, 2026 katika viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

WAFUGAJI WAHIMIZWA KUPANDA MALISHO YA MIFUGO