DKT. MADELE ATUMA UJUMBE WIKI YA MAZIWA 2026.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Fabian Madele amewataka wananchi wa mkoa wa Iringa na maeneo jirani kujitokeza kwenye maadhimisho ya kitaifa ya wiki ya maziwa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwembetogwa mkoani Iringa.

Dkt. Madele ametoa ujumbe huo Mei 29,2026 muda mfupi baada ya kukagua shughuli zinazofanywa na wadau mbalimbali wa sekta ya Mifugo waliojitokeza kwenye maonesho hayo ambapo amesisitiza kuwa lengo la Serikali ni kuhamasisha unywaji wa maziwa ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

“Mradi tuliouona mbele yetu hapa ni mkubwa na umelenga kufanya mapinduzi kwenye tasnia ya maziwa ambapo lengo lake kubwa ni kuhakikisha tunaleta ng’ombe bora wa maziwa na wafugaji wetu watapata fursa ya kufahamu teknolojia za uzalishaji wa mbegu bora” Ameongeza Dkt. Madele.

Dkt. Madele amesema kuwa maziwa ni fursa kubwa ya kiuchumi huku ikinufaisha wadau na makampuni mbalimbali yanayofanya kazi kupitia tasnia hiyo.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Fabian Madele (katikati) akipokea maelezo kuhusu maziwa yanayozalishwa na kampuni ya ASAS wakati wa ziara yake ya kuwatembelea wadau wa sekta ya Mifugo waliopo kwenye Maadhimisho ya 29 ya kitaifa ya Wiki ya Maziwa yanayofanyike kwenye Viwanja vya Mwembetogwa mkoani Iringa Mei 29,2026.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

WAFUGAJI WAHIMIZWA KUPANDA MALISHO YA MIFUGO