DKT. BASHIRU AVUTIWA NA UWEKEZAJI SEKTA YA MIFUGO LEMOTI - MONDULI
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amevutiwa na Mfugaji na Mwekezaji wa mfano Bw. Isaya Ole Mpekure anayemiliki ng'ombe zaidi ya 2,000 mitambo na ghala la kuhifadhia chakula cha mifugo ambapo shamba hilo limekuwa kitovu cha jamii ya wafugaji wa eneo hilo kuboresha mifugo yao na kufuga kwa tija.
Amesema serikali itaendelea na mikakati ya kuendeleza sekta ya mifugo ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma za chanjo na utambuzi wa mifugo ili kudhibiti magonjwa,usimamizi na uendelezaji wa ardhi ya malisho na uimarishaji wa mbegu za mifugo na miundombinu ya ufugaji ili kuongeza uzalishaji na kuwakwamua wafugaji nchini.
Kauli hiyo ya Waziri Balozi Dkt. Bashiru Juni 7, 2026 akiwa kwenye ziara yake wilayani Monduli Mkoani Arusha ziara iliyolenga kukagua utekelezaji wa shughuli za mifugo, uwekezaji wa sekta ya mifugo wa Bw. Isaya Ole Mkupure na kushiriki sherehe za kimila za jamii ya wamasai katika kijiji cha Lemote.
Katika hatua nyingine Balozi Dkt. Bashiru alisisitiza juu ya mapango wa matumizi bora ya ardhi hasa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za mifugo na kueleza mpango wa serikali wa kukabiliana na magonjwa ya mifugo ambapo tayari fedha zimeshapatikana kwa ajili ya utekelezaji wa Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo na Utambuzi wa Mifugo awamu ya pili kwa mwaka 2026/2027.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. Gloriana Kimath amesema ili kupunguza changamoto zinazowakabili wafugaji katika eneo hilo wataalam watakuwa wanawatembelea wafugaji mara kwa mara ili kutoa huduma za ugani zilizo bora zitakazowawezesha kufuga kwa tija.
Naye, Mfugaji wa mfano mwenye ng’ombe zaidi ya 2,000 Bw. Isaya Ole Mpekure amesema uwekezaji huo umekuwa na umuhimu ambapo wananchi waliokaribu wamekuwa wakichukua mbegu na kwenda kuboresha mifugo yao lakini wamekuwa wakisumbuliwa na mbung’o wanaosababisha ugonjwa wa ndorobo na kuiomba serikali kuwasaidia miundombinu ya majosho na dawa ili kuongeshea mifugo hao.
Kata ya Lemoti ina wakaazi 7,474 ambao wanajishughulisha na ufugaji kwa asilimia 80, kilimo asilimia 15 na biashara asilimia 5 na kata hiyo ina ng’ombe 12,000 kati ya hao 5,000 wamechanjwa homa ya mapafu, mbuzi na kondoo 25,000 kati ya hao 2,500 wamepata chanjo ya homa ya mapafu, kuku 1,200 na punda 1,000 ambapo kata hiyo inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa eneo la malisho kutokana na kushirikiliwa na aliyejiita mwekezaji Shamba Namba 24.




Maoni
Chapisha Maoni