DKT. BASHIRU ARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA MAONESHO YA MIFUGO

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, ameridhishwa na maandalizi kuelekea Maonesho na Mdana wa Mifugo 2026 yanayozikutanisha nchi tatu ambazo ni Tanzania, Kenya na Namibia yatakayofanyika Ubena Zomozi, ambapo Maonesho hayo yanatarajiwa kuzinduliwa kesho tarehe 19 Juni, 2026 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Akizungumza leo Juni 18, 2026 Wilayani Chalinze Mkoani Pwani, wakati akikagua Maendeleo ya Maandalizi hayo, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesema mpangilio wa Maonesho ya Mifugo umekaa vizuri, na amewapongeza wadau mbalimbali walioshiriki kuandaa Maonesho hayo ambayo yatafungua fursa kwa wafugaji nchini.

"Maonesho haya ni fursa kwa wafugaji kwani wataweza kujifunza jinsi ya kufuga kisasa na kwa tija, na kupata elimu mbalimbali kuhusu Malisho ya Mifugo" amesema Mhe. Balozi Dkt. Bashiru 

Aidha, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameipongeza Menejimenti ya Wizara kwa Maandalizi mazuri ya Kilimo cha Malisho, ambapo amewataka Watendaji wa Wizara kutoa elimu ya kutosha kwa wafugaji kuhusu Malisho hayo na matumizi ya Teknolojia mpya ya ufugaji.

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Maeneo ya Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo (DGLF), Dkt. Asimwe Rwiguza (wa nne kushoto), akimuonesha Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (wa tatu kushoto), aina za Malisho yaliyopandwa katika Maeneo ya Maonesho na Mnada wa Mifugo katika Ranchi ya Mbogo Ubena Zomozi, wakati alipotembelea na kukagua maandalizi ya Maonesho hayo, Juni 18, 2026, Chalinze - Pwani.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (wa pili kulia), akizungumza na Watendaji Wakuu wa Ranchi ya Mbogo, wakati alipotembelea kukagua maandalizi ya Maonesho na Mnada wa Mifugo yaliyopo Ubena Zomozi, Juni 18, 2026, Chalinze - Pwani, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ranchi hiyo, Bw. Naweed Mulla.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (wa kwanza kushoto), akikagua Mazizi na Mifugo, katika eneo la Maonesho na Mnada wa Mifugo katika Ranchi ya Mbogo Ubena Zomozi, Juni 18, 2026, Chalinze - Pwani.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

WAFUGAJI WAHIMIZWA KUPANDA MALISHO YA MIFUGO