BIMA YA KIDIGITALI YA MIFUGO YAZINDULIWA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Kisaka Meena, amezindua Bima ya Kidigital ambayo imewezeshwa kwa ushirikiano baina ya Kampuni ya Bima ya CRDB pamoja na Kampuni ya ACRE Africa ambayo itatumia teknolojia ya kisasa kulinda mali za wafugaji nchini.

Akizungumza leo Juni 29, 2026, katika Uzinduzi wa Bima ya Kidigitali ya Mifugo ijulikanayo kama Smart Mifugo, katika Hoteli ya Serena iliyopo Jijini Dar es Salaam, Bi. Meena amesema katika kukabiliana na changamoto za wafugaji, Kampuni ya Bima ya CRDB pamoja na Kampuni ya ACRE Africa, zimeleta suluhisho la ubunifu ambalo linatumia teknolojia ya kisasa kulinda mali za wafugaji wetu kupitia Smart Mifugo, na wafugaji kwa sasa wanaweza kupata bima kwa urahisi zaidi kwa njia ya kidijitali, salama na yenye uwazi.

"Nimejulishwa kuwa kutakuwa na mfumo wa DigiBima App unaorahisisha usajili, malipo ya bima, na uwasilishaji wa madai, ambayo ni hatua muhimu katika kupeleka huduma karibu zaidi na wananchi, hususan wafugaji walioko vijijini, na hatua hii ni muhimu kwani inalenga kuleta mapinduzi makubwa katika Sekta ya Mifugo hapa nchini." amesema Bi. Meena.

Aidha, Bi. Meena ameweka bayana kuwa teknolojia ya Akili Mnemba itatumika katika kutambua mifugo kupitia alama ya kipekee ya pua ya mnyama, na hiyo ni hatua muhimu na kubwa katika kuendeleza Sekta ya Mifugo kwa kutumia teknolojia za kisasa, na ametoa wito kwa wafugaji wote nchini kutumia teknolojia hiyo, kwani inaleta fursa ya kulinda mifugo yao ambayo ni mali muhimu na tegemeo lao la maisha.

Bi. Meena pia amesisitiza matumizi ya teknolojia hizo kwa ufanisi, weledi na ufasaha ili kuongeza tija, kuboresha utambuzi wa mifugo na kuimarisha usimamizi wa Sekta kwa ujumla, na amebainisha kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Sekta binafsi ili ziendelee kuleta ubunifu utakaoongeza tija katika uzalishaji na kuboresha maisha ya wananchi.

Bi. Meena amezipongeza CRDB Group na ACRE Africa kwa kuendelea kuwa vinara wa ubunifu katika Sekta ya fedha, pamoja kwa utaalamu katika teknolojia na usimamizi wa vihatarishi katika Sekta za kilimo na Mifugo, na amesema ni matarajio ya Serikali kwamba wadau wote zikiwemo taasisi za kifedha, vyama vya ushirika, na wafugaji wenyewe wataitumia fursa hiyo kikamilifu ili kuboresha uzalishaji, kupunguza hasara, na kuongeza kipato. 

Kwa upande wake, MKurugenzi Mtendaji Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela amesema ubunifu huo wa Bima ya Mifugo una faida nyingi kibiashara na sululisho la changamoto wa wafugaji na wafanya biashara.

Dkt. Nsekela amesema kupitia CRDB wafugaji na wafanyabiashara za mifugo watawezeshwa kupata mitaji ya kununua ng’ombe, kuuza ng’ombe na kununua maziwa kwa ajili kukuza biashara zao ili kukuza vipato vyao, na ndio mana CRDB wamepanga kuwafikia wafugaji Tanzania nzima.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima CRDB, Bw. Wilson Mnzava amefafanu kuwa bidhaa nyingi za mifugo zinaharibiwa ikiwemo ngozi za mifugo ambazo uwekwa nembo na wafugaji kama ishara ya kutambua mifugo yao, ila kupitia Bima ya Kidigital ya Mifugo wafugaji wataweza kuwatambua mifugo yao kwa kutumia utambuni wa pua ambao unatumia Akili Mnemba.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Kisaka Meena, akihutubia wadau wa Sekta ya Mifugo, katika hafla ya Uzinduzi wa Bima ya Kidigitali ya Mifugo ijulikanayo kama Smart Mifugo, iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, 29 Juni, 2026, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Kisaka Meena (wa tatu kulia), akizindua Bima ya Kidigitali ya Mifugo ijulikanayo kama Smart Mifugo, katika hafla ya Uzinduzi wa Bima hiyo, iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, 29 Juni, 2026, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Kisaka Meena (kushoto), akikabidhiwa zawadi, katika hafla ya Uzinduzi wa Bima ya Kidigitali ya Mifugo ijulikanayo kama Smart Mifugo, iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, 29 Juni, 2026, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Kisaka Meena (aliyesimama katikati), akiwa kwa picha ya pamoja na Wadau wa Sekta ya Mifugo pamoja na Wataalam wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, katika hafla ya Uzinduzi wa Bima ya Kidigitali ya Mifugo ijulikanayo kama Smart Mifugo, iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, 29 Juni, 2026, Dar es Salaam, wa tatu kulia ni MKurugenzi Mtendaji Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela, na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima CRDB, Bw. Wilson Mnzava.

Wadau wa Sekta ya Mifugo wakiwa katika hafla ya Uzinduzi wa Bima ya Kidigitali ya Mifugo ijulikanayo kama Smart Mifugo, iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, 29 Juni, 2026, Dar es Salaam.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UTEKELEZAJI WA UFUGAJI SAMAKI KWA VIZIMBA WAANZA ZIWA TANGANYIKA

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI