WASHIRIKI WA MAFUNZO YA UONGOZI NA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA PWANI WATAKIWA KUSIMAMIA RASILIMALI ZA BAHARI KWA UWAZI NA USAWA

Na. Maria Mtambalike

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Mafunzo,Tafiti na Huduma za Ugani Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw Samwel Mdachi wakati akifunga mafunzo ya uongozi na usimamizi wa rasilimali za pwani kwa washiriki 12 waliopata mafunzo kwa siku 14 kuanzia tarehe 8 April mpaka  tar 21 April 2026 katika chuo cha Uvuvi FETA. 

Bw Mdachi amesema kuwa mafunzo haya hayatakuwa na maana kama washiriki hawatafanya kazi zao kwa ubora na kwa vitendo zaidi huku akiwataka watumie mbinu walizojifunza kutatua migogoro kwa amani.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Dkt Semvua Mzighani ambao wameendesha mafunzo hayo kwa kushirikiana na Shirika la IUCA kupitia mradi wa  Re sea amesema FETA itaendelea kushirikiana na  wadau mbalimbali katika utoaji wa elimu katika jamii.

Naye Mwakilishi kutoka IUCN ambae ni meneja wa program ya uhifadhi wa bahari Bw Joseph Orila amesema kuwa lengo la mradi wao ni kutoa mafunzo kwa washiriki/wakufunzi ambao watakwenda kusimamia mafunzo kwa washiriki wengine katika maeneo ya pwani ya pemba na Tanga ili kuongeza maarifa,ujuzi,umahiri na kuboresha usimamizi wa rasilimali za pwani.

Awali akiongea Mratibu wa mafunzo hayo kutoka FETA Dkt Milali Machumu amesema kuwa mafunzo haya yamelenga kuimarisha uongozi na mifumo ya kiutawala katika maeneo ya Tanga na pemba lengo likiwa ni kuziwezesha jamii za pwani ili ziweze kusimamia rasilimali zetu. 

Katika hafla hiyo Mgeni rasmi alizindua Mtaala pamoja na  muongozo wa mafunzo ya uongozi na usimamizi wa rasilimali za pwani.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO