UHABA WA MALISHO YA MIFUGO UNAVYOMNYIMA USINGIZI DKT. BASHIRU

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (Mb) amesema ili kumaliza changamoto ya uhaba wa malisho ya mifugo, wafugaji lazima wawe na usimamizi mzuri wa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika kuzalisha malisho yatakayokidhi mifugo yao.

Mhe. Balozi Dkt. Bashiru ameeleza hayo wakati alipotembelea Shamba la kuzalisha Malisho la Langwira Mbarali Mkoani Mbeya Mei 03, 2026 ambapo ameeleza kuwa ukosefu wa malisho  ya mifugo kwa wafugaji hasa kipindi cha kiangazi umekuwa ukimnyima usingizi kutokana na adha wanayopata wafugaji nchini.

“Nilikuwa Sijui kama Mawaziri wa Mifugo na Uvuvi huwa hawalali kwa sababu ya wafugaji kukosa malisho,mimi kikianza Kiangazi silali, suluhu ipo katika uzalishaji wa malisho, kwa hiyo ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi lazima tuwe na mpango mzuri wa matumizi bora ya ardhi, tuzalishe kisasa malisho halafu wakati wa kiangazi tuyatumie malisho yaliyohifadhiwa wakati wa  masika” alisema Mhe. Dkt. Bashiru.

Pia, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesisitiza kuwa ili  kukabiliana na changamoto ya malisho nchini wafugaji wanapaswa kufuga kisasa kwa kupunguza idadi ya mifugo na kuzalisha malisho.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (wapili kulia) akikagua jinsi utengenezaji wa Hay katika Shamba la Malisho ya  la Langwira lililopo Wilayani Mbarali Mkaoni Mbeya wakati wa Ziara  yake  Mei 03, 2026.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akikagua Shamba la Malisho ya  la Langwira lililopo Wilayani Mbarali Mkaoni Mbeya wakati wa Ziara  yake  Mei 03, 2026.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (wa saba, kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wataalam wa  Shamba la Malisho la Langwira lililopo Wilayani Mbarali Mkaoni Mbeya wakati wa Ziara  yake  Mei 03, 2026.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO