HUDUMA ZA MATIBABU NA ELIMU YA USTAWI WA PUNDA ZAANZA KUTOLEWA GEITA

Na Chiku Makwai-Geita, 

Wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na taasisi zilizo chini yake, kwa kushirikiana na Shirika la INADES-Formation Tanzania na Shirika la ASPA, wameanza  zoezi la kliniki ya matibabu kwa mnyama punda linaloambatana na utoaji wa elimu kuhusu ustawi wa punda katika vituo vya Magogo, Magenge na Mgusu mkoani Geita.

Zoezi hilo linalofanyika kwa siku tatu lina lenga kuwapatia wafugaji na watumiaji wa punda elimu kwa vitendo kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia bora za vifaa vya kazi, huduma za afya pamoja na utunzaji bora wa punda ili kuongeza ustawi na tija ya mnyama huyo.

Aidha, wataalamu hao wametoa huduma mbalimbali za matibabu kwa punda ikiwemo uchunguzi wa afya, tiba na ushauri wa namna bora ya kuwahudumia wanyama hao ili kuepusha magonjwa na mateso yasiyo ya lazima.

Zoezi hilo limeanza Mei 6, 2026 na linatarajiwa kuhitimishwa kesho Mei 8, 2026 sambamba na maadhimisho ya Siku ya Punda Kitaifa yatakayofanyika mkoani Geita ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Martin Shigela.

Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni; “Kulinda Punda wa Afrika ni Wajibu Wetu Sote.”







Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO