RAIS SAMIA ATAZINDUA MELI YA UVUVI WA BAHARI KUU APRILI 25, 2026 - DKT BASHIRU

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani anatarajiwa kuzindua Meli ya Kwanza ya Uvuvi wa Bahari Kuu, ambapo uzinduzi wake utafanyika Makao Makuu ya 

Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesema hayo Aprili 17, 2026, wakati wa ziara ya  Kamati ya Uchumi na Uwekezaji ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kutembelea na kukagua ujenzi wa bahari ya uvuvi Kilwa Masoko Mkoani Lind na kuieleza kamati hiyo kuwa  bandari ya uvuvi Kilwa masoko iliyogharimu shilingi bilioni 280 baada ya kukamilika itafanyiwa majaribio kabla ya kukabidhiwa kwa serikali.

“ Mradi huu kwa sawa  tuko asilimia 97, asilimia tatu zilizobaki ni kwa sababu kuna mitambo mingine imeagizwa ili ifungwe halafu tufanye majaribio kabla ya kukabidhiwa, wakati wowote ndani ya mwezi wa nne na watano mkandarasi anaweza kutukabidhi” alisema Mhe. Balozi Dkt. Bashiru.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Uwekezaji ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Makame Mohammed Sufiani amepongeza maono ya Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Mwinyi kwa kujana na maono ya ujenzi wa bandari ya uvuvi itakayochochea ukuaji wa sekta ya uvuvi na uchumi wa buluu.

Naye Naibu Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe. Mboja Ramadhan Mshenga amesema baada ya kujifunza kuhusu  ujenzi wa bandari ya uvuvi eneo la Kilwa Masoko na Zanzibar pia itajenga bandari ya uvuvi ili kukuza uchumi wa buluu.

Ziara hiyo pia imehudhuriwa na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Uvuvi (KKB -VBKM) Mhe. Livingstone Lusinde aliyeambatana na Wajumbe wawili wa Kamati hiyo.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akielezea hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko iliyopo Mkoa wa Lindi, wakati wa ziara ya Kamati ya Uchumi na Uwekezaji ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar  Aprili 17, 2026.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (watatu kulia) akiwaonesha Wajumbe wa Kamati ya Uchumi na Uwekezaji ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Miundombinu ya Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko wakati wa Ziara ya kamati hiyo iliyofanyika Aprili 17, 2026

Wajumbe wa Kamati ya Uchumi na Uwekezaji ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi baada ya ukaguzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko, wengine walioambatana na Waziri ni baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo pamoja na wataalam wa Wizara na Ofisi ya Mkoa wa Lindi.

Mwonekano wa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa Masoko ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 97%.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO