PROF. SHEIKH AELEKEZA UZALISHAJI WA VIFARANGA KUANZIA 200,000 KILA MWEZI KUFIKIA JUNI 2026

Na. Chiku Makwai, WMUV

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Prof. Mohammed Sheikh, amezitaka taasisi za Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kuimarisha ushirikiano ili kufikia uzalishaji wa vifaranga vya samaki kuanzia 200,000 hadi 300,000 kwa mwezi ifikapo Juni 2026.

Maelekezo hayo aliyatoa Aprili 14, 2026, wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa Wizara pamoja na taasisi hizo, kilichofanyika katika ofisi za TAFIRI mkoani Kigoma.

Prof. Sheikh alisisitiza kuwa lengo la uzalishaji huo ni kurahisisha upatikanaji wa vifaranga bora kwa vijana wanaonufaika na mikopo ya vizimba, pamoja na wananchi wengine wanaojihusisha na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba katika Ziwa Tanganyika.






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO