MIFUMO YA TAARIFA ZA UVUVI NA UFUATILIAJI NA TATHIMINI KUIMARISHWA
Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya kaa Kikao kazi ili kuimarisha mipango ya mifumo ya taarifa za uvuvi, ufuatiliaji na tathmini kupitia Mradi wa Kukuza Usimamizi Endelevu wa Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji wa Bahari Tanzania (TASFAM), kikao kinachofanyika Mjini Morogoro, na kinaendelea leo ili kubaini mapungufu na kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha mifumo ya taarifa na takwimu.
Kikao hicho kimefunguliwa rasmi jana (14.04.2026) na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena, ambaye amebainisha juhudi mbalimbali zinazotekelezwa chini ya idara na taasisi zitasaidia kuepusha urudiaji wa kazi, kuongeza ufanisi na kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali fedha, watu na muda.









Maoni
Chapisha Maoni