KAMANI AELEZA MKAKATI WA SERIKALI KUONGEZA MAENEO YA WAFUGAJI NNCHINI
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ng’wasi Damas Kamani amesema Serikali inaendelea kutenga, kupima na kumilikisha kwa wafugaji maeneo ya shughuli za ufugaji kutoka hekta Milioni 3.46 hadi hekta Milioni 6 pamoja na kuyaboresha maeneo hayo kwa kuyapatia huduma muhimu zikiwamo maji, majosho, malisho na huduma za ugani.
Hatua hiyo ya kutenga maeneo ya shughuli za ufugaji ni utekelezaji wa maelekezo ya Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wakati wa Kufungua Rasmi Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dodoma, Novemba 14, 2025 pamoja na Maelekezo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2025.
Mhe. Kamani amesema hayo leo Aprili 21, 2026 vacati akijibu Swali la Mbunge wa Kalambo Mkoani Rukwa Mhe. Edifonsi Joackim Kanoni aliyehoji kuwa serikali ina mango gani wa kuongeza ardhi ya kilimo kwa wananchi wa kata ya Mkoe na Mbuluma kutoka katika eneo la NARCO.
“Mheshimiwa Spika, Ranchi ya Kalambo ni moja kati ya ranchi 15 zinazomilikiwa na Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO). Ranchi hii inapatikana katika Wilaya za Nkasi na Kalambo, Mkoani Rukwa. Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, ranchi imepakana na Kata za Mkoe na Mbuluma, ambapo kuna Kijiji cha Katapulo (Kata ya Mkoe) na Vijiji vya Mbuluma na Lolesha (Kata ya Mbuluma)” alisema Mhe. Kamani.
Ameongeza kuwa, Kwa sasa Serikali kupitia Ranchi ya Kalambo haina eneo la ziada na la kutosha kwa ajili ya kuwezesha shughuli zingine kwa wahitaji kutoka katika Kata za Mkoe na Mbuluma kwa ajili ya kilimo, kwa kuwa maeneo yote yaliyotengwa kwa sasa yana matumizi mahususi yanayoendelea na kutoa rai kwa Halmashauri zote hapa nchini kuhakikisha kutenga, kupima, kumilikisha kulinda na kuhifadhi maeneo yote ya kimkakati yaliyotegwa kwa shughuli za mifugo.
Ranchi ya Kalambo ina jumla ya hekta 64,651 Kati ya hizo, eneo la ranchi mama ni hekta 12,167 na eneo lililobaki la hekta 52,484 likijumuisha vitalu 31 ambavyo vimepangishwa kwa wananchi ambapo Kati ya vitalu hivyo, vitalu viwili (2) vimepangishwa kwa wananchi wa Kijiji cha Mbuluma ambacho kina kitalu cha ukubwa wa hekta 3,167.4 na Kijiji cha Lolesha chenye kitalu cha ukubwa wa hekta 2,107.

Maoni
Chapisha Maoni