WAVUVI TANGA WAPEWA ELIMU YA UZALISHAJI ZAO LA MWANI NA JONGOO BAHARI

Na. Stanley Brayton, WMUV

Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2025/2026 imeanza utekelezaji wa Mradi wa Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM) kwa kuwajengea uwezo katika mnyororo wa thamani wakulima wa mwani na wakuzaji Jongoo Bahari, Mradi ambao unatekelezwa kwa miaka mitano (2025 hadi 2030), wenye lengo kuimarisha Usimamizi wa Rasilimali za Baharini na kuboresha maisha ya jamii za pwani Tanzania Bara na Zanzibar.

Akizungumza leo Machi 26, 2026 Jijini Tanga kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari Jijini hapo, Afisa Uvuvi Mkuu wa Wizara hiyo, Ndg. Silas William, amesema Mafunzo hayo ni fursa adhimu kwa Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari kwani wanapata kujifunza kuhusu Mnyororo mzima wa thamani wa Mazao hayo ambayo yenye tija kwa soko la sasa.

"Wizara kwa sasa imekuja na Mpango madhubuti wa kuwaelimisha Wakulima ili waweze kufanya shughuli zao za uzalishaji kwa vikundi na ushirika, na hatimae kuhakikisha kwamba Soko la Mwani na Jongoo Bahari linakuwa na mashiko ndani na nje ya nchi ili kukuza Uchumi binafsi na Taifa kiujumla." amesema Ndg. Silas.

Aidha, Ndg. Silas amewataka Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari kukuza Jongoo Bahari kwa wingi na kujiunga kwenye vikundi na vyama vya Ushirika ili waweze kunufaika zaidi kwa kupata mikopo ambayo inalenga kuwainua Wakulima wa Mazao ya Uvuvi.

Naye, Mwenyekiti wa Mtaa wa Sahare Kijijini ambaye pia ni Mkulima wa Mwani, Bw. Amiri Makalamange, ameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwapatia vitendea kazi vya kisasa kwa ajili ya kuzalisha Mwani na Jongoo Bahari pamoja na mbegu za Jongoo Bahari na Masoko ya bidhaa hizo za Uvuvi ambayo yatawasaidi kuuza bidhaa zao.

Vilevile, Bw. Makalamange ameelezea changamoto mbalimbali zinazowakumba wavuvi na wakulima wa Mwani wa eneo hilo na kuwaomba Wizara kuwasaidia boti za ulinzi shirikishi ili kuimarisha hali ya ulinzi katika maeneo hayo.


Afisa Uvuvi Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ndg. Silas William, akitoa neno la Utangulizi na kuelezea lengo la Wizara katika kutoa elimu kwa wakulima wa mwani, wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo wa Mnyororo wa Thamani Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, elimu inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), katika Kata ya Mzingani, Machi 26, 2026 Tanga Jiji.

Afisa Uvuvi Mwandamizi Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Fatuma Juma, akifafanua na kuelezea Mwongozo wa Ufugaji wa Jongoo Bahari, wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo wa Mnyororo wa Thamani Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, elimu inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), katika Kata ya Mzingani, Machi 26, 2026 Tanga Jiji.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Sahare Kijijini ambaye pia ni Mkulima wa Mwani, Bw. Amiri Makalamange, akielezea changamoto zinazowakumbwa na kuiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi vitendea kazi vya kuzalisha Mwani na Jongoo Bahari, na Masoko ya bidhaa hizo za Uvuvi, wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo wa Mnyororo wa Thamani Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, elimu inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), katika Kata ya Mzingani, Machi 26, 2026 Tanga Jiji.


Picha ni Wakulima wa Mwani wakisikiliza Mafunzo, wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo wa Mnyororo wa Thamani Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, elimu inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), katika Kata ya Mzingani, Machi 26, 2026 Tanga Jiji.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO