UHIMILISHAJI WA MIFUGO KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZIWA NCHINI
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaendelea kutekeleza Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP) unaolenga kuongeza uzalishaji wa maziwa na nyama kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya uhimilishaji.
Kauli hiyo imetolewa leo Machi 23, 2026 na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Stephen Michael, wakati akifungua mafunzo ya uhimilishaji kwa wataalamu wa mifugo yaliyofanyika katika Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC) mkoani Arusha.
kuongeza tija na kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.
“Mafunzo haya ni sehemu muhimu ya kuhakikisha wataalamu wanapata ujuzi wa kisasa utakaowawezesha kuwahudumia wafugaji kwa ufanisi zaidi ili kuongeza tija na kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi,” amesema Bw. Michael.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC) Dkt. Dafay Bura amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea wataalam wa mifugo uwezo ili kusaidia wafugaji kuboresha mbari za mifugo itakayosaidia kuongeza uzalishaji wa maziwa na nyama nchini.
Naye Afisa Uzalishaji na Afya ya Wanyama kutoka Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP) Bi. Patricia Ngoda ameeleza kuwa mradi huo utawapatia vifaa vitakavyowasaidia kuwafikiwa wanufaika kwa haraka zaidi pamoja na uwasilishaji wa taarifa za takwimu za mradi kwa njia ya kidijitali.
Pamoja na mafunzo hayo kwa wataalam wa mifugo mradi huo pia utatoa vifaa vya uhimilishaji, pikipiki pamoja na vifaa vya kidigitali kwa ajili kuongeza uzalishaji na thamani ya mazao ya mifugo.




Maoni
Chapisha Maoni