Na. Edward Kondela
Mradi wa Uendelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), umepongezwa kwa hatua uliyofikia kwenye utekelezaji wake, katika kuhakikisha unaboresha maisha ya wananchi wa Ukanda wa Bahari ya Hindi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, amebainisha hayo (26.03.2026), wakati akipatiwa taarifa ya tathmini ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo wa miaka mitano, ambapo amesema ni muhimu uakisi maisha ya wavuvi na wadau wengine wa sekta ya uvuvi.
Ameongeza kuwa miradi itakayojengwa kupitia TASFAM ni muhimu ikamilike kwa wakati sambamba na thamani ya fedha zinazotolewa ili iwe na tija kwa wananchi badala ya kuchukua muda mrefu huku ikitumia fedha nyingi.
“Ninazitaka taasisi na idara zilizo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi zinazotekeleza mradi wa TASFAM kuhakikisha shughuli zilizopangwa kwenye maeneo yao zinafanyika kama zilivyopangwa na kuhakikisha serikali inapata mapato na kunufaisha wananchi hususan wadau wa sekta ya uvuvi.” Amesema Mhe. Balozi Dkt. Bashiru
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Prof. Mohammed Sheikh amesema vifaa vya kisasa ni muhimu katika Maabara ya Taifa ya Uvuvi (NFQCLAB).
Pia, amesema licha ya uwepo wa vifaa hivyo ni muhimu wataalamu wakazidi kujengewa uwezo ili sampuli mbalimbali za mazao ya uvuvi ziwe zinafanyiwa utafiti hapa nchini badala ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.
Baadhi ya wakuu wa taasisi na idara zinazotekeleza mradi wa TASFAM, wamemuhakikishia Waziri wa Mifugo na Uvuvi, kwamba watafanya kila jitihada ili kufikia malengo yanayotarajiwa kama walivyokubaliana kupitia mkopo wa Benki ya Dunia.
Mradi wa TASFAM unatekelezwa hapa nchini kwa wadau wa sekta ya uvuvi katika Ukanda wa Bahari ya Hindi kwenye mikoa mitano, katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2025 hadi 2030 kwa thamani ya Dollar za Kimarekani Milioni 117.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, akifafanua na kupongeza hatua za utekelezaji katika Mradi wa Uendelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), kwenye kikao cha tathmini kilichofanyika katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jjini Dodoma. (26.03.2026)
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Prof. Mohammed Sheikh, akielezea umuhimu wa vifaa vya kisasa na kuwajengea uwezo wataalamu wa Maabara ya Taifa ya Uvuvi (NFQCLAB), kwenye kikao cha tathmini ya Mradi wa Uendelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), kilichofanyika katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jjini Dodoma. (26.03.2026)
Mratibu wa Mradi wa Uendelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM) Tanzania Bara Dkt. Nichrous Mlalila, akitoa maelezo ya tathmini ya mradi huo unaotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2025 hadi 2030 kwenye mikoa mitano ya Ukanda wa Bahari ya Hindi. Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jjini Dodoma. (26.03.2026)
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi Agnes Meena akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo anayesimamia Mifugo Dkt. Fabian Madele, wakati wa kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), kilichofanyika katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jjini Dodoma. (26.03.2026)
Meneja wa Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) Dkt. Emmanuel Sweke, akichangia hoja mbalimbali na kuahidi kufuatilia madeni inayodai hifadhi hiyo, wakati wa kikao cha tathmini ya Mradi wa Uendelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), kilichofanyika katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jjini Dodoma. (26.03.2026)
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ismael Kimirei, akiainisha hatua zilizofikiwa za kufanya tafiti za kuweka vizimba kwenye Bahari ya Hindi, wakati wa kikao cha tathmini ya Mradi wa Uendelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), kilichofanyika katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jjini Dodoma. (26.03.2026)
Muoneakano wa picha ya washiriki wa kikao cha tathmini ya Mradi wa Uendelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), kilichofanyika katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jjini Dodoma, kikiongozwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa. (26.03.2026)
Maoni
Chapisha Maoni