Na. Stanley Brayton, WMUV
Afisa Uvuvi Mwandamizi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Fatuma Rajabu Juma amebainisha fursa mbalimbali za ukuzaji wa jongoo bahari, ambapo amewashauri wakulima wa jongoo bahari kukuza zao hilo la Uvuvi kwa wingi ili kujiongezea kipato, kwani masoko ya Jongoo Bahari yapo kuanzia ndani na nje ya nchi.
Akizungumza leo Machi 27, 2026 Jijini Tanga wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo wakulima wa mwani na jongoo bahari, elimu inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), Bi. Fatuma amesema jongoo bahari ni fursa adhimu na zao lenye tija kubwa kiuchumi na lina faida kubwa kwa walaji na wafanyabiashara kutokana na uhitaji wake mkubwa, ambapo kilo moja ya jongoo bahari huuzwa kati ya shilingi 75,000 hadi 150,000.
“Katika nchi mbalimbali, jongoo bahari hutumika kuboresha afya na kusaidia kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza,” amesema Bi. Fatuma.
Aidha, Bi. Fatuma amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa fedha kupitia programu ya Vijana wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT), ili kuwawezesha vijana kukuza viumbe maji bila changamoto na kujipatia kipato, ambapo mojawapo ya wanufaika wa mikopo hiyo ni wakuzaji wa jongoo bahari.
Vilevile, Bi. Fatuma amewataka wakulima kuongeza uzalishaji wa jongoo bahari ili kujiongezea kipato, akibainisha kuwa jongoo bahari huchukua takribani miezi nane hadi kumi kufikia hatua ya kuvunwa na kuingia sokoni.
Pia, Bi. Fatuma amewashauri wakulima kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalam kuhusu mnyororo mzima wa ufugaji wa jongoo bahari, ikiwa ni pamoja na uchaguzi sahihi wa eneo, aina ya jongoo, chakula chao, uangalizi wa mara kwa mara pamoja na mbinu bora za uvunaji na uhifadhi ili kuhakikisha ubora wa bidhaa na kuongeza thamani sokoni.
Afisa Uvuvi Mwandamizi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Fatuma Rajabu Juma, akielezea namna ya kutunza na kukuza Jongoo Bahari kutoka kuwatunza hadi kuwavuna, wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo wa Mnyororo wa Thamani Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, elimu inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), katika Kata ya Tongoni, Machi 27, 2026 Tanga Jiji.
Mkulima wa Mwani, Bi. Time Mohammed (aliyeinua Mkono), akiuliza swali kuhusiana na namna ya uhifadhi wa Mwani baada ya kuvunwa, wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo wa Mnyororo wa Thamani Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, elimu inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), katika Kata ya Tongoni, Machi 27, 2026 Tanga Jiji.
Afisa Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Robert Nicholaus, akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa Wakulima wa Mwani na Jongoo kuhusiana na Mnyororo wa Thamani wa Mwani na Jongoo Bahari, wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo wa Mnyororo wa Thamani Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, elimu inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), katika Kata ya Tongoni, Machi 27, 2026 Tanga Jiji.
Afisa Uvuvi wa Kata ya Tongoni, Bw. Anney Nyirenda (anaeongea kwa ishara ya Mikono), akifafanua baadhi ya changamoto zinazowakumbwa Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari na kuiomba Wizara kuwasaidia kuzitatua ikiwemo ufinyu wa vitendea kazi, wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo wa Mnyororo wa Thamani Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, elimu inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), katika Kata ya Tongoni, Machi 27, 2026 Tanga Jiji.
Maafisa wa Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakiandika maoni mbalimbali ya Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo wa Mnyororo wa Thamani Wakulima wa Mwani na Jongoo Bahari, elimu inayotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), katika Kata ya Tongoni, Machi 27, 2026 Tanga Jiji, wa pili kushoto niAfisa Uvuvi Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ndg. Silas William.
Maoni
Chapisha Maoni