Nav bar

Jumanne, 27 Januari 2026

VCT YASAJILI WATAALAM WA MIFUGO 293 WENYE SIFA STAHIKI

Na. Stanley Brayton, WMUV

Vituo 130 vya Huduma za Afya ya Wanyama vysajiliwa.

Baraza la Veterinari Tanzania (VCT) limekamilisha mapitio na kusajili Wataalam wa Wanyama wenye sifa stahiki, pamoja na kusajili Vituo mbalimbali vya kutoa Huduma za Afya ya Wanyama, ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Sheria ya Veterinari SURA 319.

Akizungumza katika Kikao cha 62 cha Baraza cha kujadili utekelezaji wa shughuli za Baraza hilo kwa Robo ya pili ya mwaka wa 2025/2026, leo Januari 27, 2026 Dodoma, Mwenyekiti wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT), Prof. Lughano Kusiluka amesema Baraza limepitia na kuridhia kuwapa usajili watoa Huduma za Afya ya Wanyama 293 na Vituo 130 vya utoaji Huduma za Afya ya Wanyama.

“usajili huu umefanyika kwa kuzingatia Sheria ya Veterinari SURA 319, kwa kuangalia vigezo mbalimbali stahiki.” amesema Prof. Kusiluka

Aidha, Prof. Kusiluka amewataka Wataalam hao na Vituo hivyo kutoa Huduma hizo kwa uweledi na utaalam kwa wafugaji na kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi katika kutoa Huduma hizo ambazo zimewekwa katika Sheria ya Veterinari.

Vilevile, Prof. Kusiluka amewataka wafugaji kuwatumia Wataalam hao ambao wamesajiliwa  na Baraza kwa kufuata Sheria ili kuepukana na athari ambazo zinaweza kuleta madhara katika Mifugo yao, yatokanayo na Wataalam wasiosajiliwa.

Kwa Upande wake, Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT) ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Dkt.  Amani Kilemile amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Waziri wake mwenye dhamana, Mhe. Bashiru Ally Kakurwa inaendelea kuhakikisha kuwa wafugaji na Mifugo wanapata Huduma Bora ambayo inatolewa na Wataalam ambao wamethibitishwa na kupewa Usajili pamoja na leseni kutoka Mamlaka husika.


Mwenyekiti wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT), Prof. Lughano Kusiluka, akielekeza jambo kwa Wajumbe wa Baraza hilo kuhusu Usajili wa Wataalam wa Huduma za Afya ya Wanyama, katika Kikao cha 62 cha Baraza cha kujadili utekelezaji wa shughuli za Baraza hilo kwa Robo ya pili ya mwaka wa 2025/2026, kilichofanyika katika Ukumbi wa Royal Village, Januari 27, 2026 Dodoma.

Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT) ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Dkt. Amani Kilemile, akielezea hali ya maombi ya Vituo vya kutolea Huduma za Afya ya Wanyama, katika Kikao cha 62 cha Baraza cha kujadili utekelezaji wa shughuli za Baraza hilo kwa Robo ya pili ya mwaka wa 2025/2026, kilichofanyika katika Ukumbi wa Royal Village, Januari 27, 2026 Dodoma.

Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Nchini, Dkt. Benezeth Lutege, akichangia hoja, katika Kikao cha 62 cha Baraza cha kujadili utekelezaji wa shughuli za Baraza hilo kwa Robo ya pili ya mwaka wa 2025/2026, kilichofanyika katika Ukumbi wa Royal Village, Januari 27, 2026 Dodoma.

Wakili Mwandamizi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bi. Mariam Haji, akitoa ushauri wa kisheria katika kupitisha maombi ya Wataalam na Vituo vya Huduma za Afya ya Wanyama, katika Kikao cha 62 cha Baraza cha kujadili utekelezaji wa shughuli za Baraza hilo kwa Robo ya pili ya mwaka wa 2025/2026, kilichofanyika katika Ukumbi wa Royal Village, Januari 27, 2026 Dodoma.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT) wakipitia Orodha na maombi ya Vituo mbalimbali vya kutolea Huduma za Afya ya Wanyama, wakiwa katika Kikao cha 62 cha Baraza cha kujadili utekelezaji wa shughuli za Baraza hilo kwa Robo ya pili ya mwaka wa 2025/2026, kilichofanyika katika Ukumbi wa Royal Village, Januari 27, 2026 Dodoma.

Picha ni baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT) wakiwa katika Kikao cha 62 cha Baraza cha kujadili utekelezaji wa shughuli za Baraza hilo kwa Robo ya pili ya mwaka wa 2025/2026, kilichofanyika katika Ukumbi wa Royal Village, Januari 27, 2026 Dodoma.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni