Nav bar

Alhamisi, 9 Oktoba 2025

WADAU WAHIMIZWA UMOJA UTUNZAJI RASILIMALI ZA UVUVI

 Ikiwa ni siku ya pili ya warsha ya kujadili ujumuishwaji wa masuala ya bioanuwai katika usimamizi wa rasilimali za uvuvi wadau wa maendeleo ya sekta ya uvuvi wamehimizwa kuwa na nguvu za pamoja zitakazosaidia kulinda na kutunza rasilimali za bahari na vyanzo vingine vya maji kwa ajili ya shughuli za uvuvi.

Hayo yameelezwa Oktoba 8, 2025 katika Hoteli ya Giraffe Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Mhina ambapo amesema serikali na wadau wengine wa maendeleo waweke  jitihada za pamoja katika utunzaji wa  mazingira ya viumbe maji itasaidia kuwa na uvuvi endelevu na kuinua uchumi wa jamii.

Amehimiza washiriki wa warsha hiyo kutumia jukwaa hilo ili kubadilisha mtazamo kuhusu utunzaji wa mazingira ya bahari, vyanzo vya maji na rasilimali za uvuvi ili jamiii iweze kunufaika na sekta ya uvuvi  endelevu na kuondokana na umaskini.

Aidha, Katika siku ya pili ya warsha hiyo majadiliano mbalimbali yamefanyika yakiwa na lengo la kuja na mpango mkakati  utakaosaidia kufanya ujumuishaji wa masuala ya bioanuwai katika usimamizi wa sekta ya uvuvi.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Mhina akihimiza ushirikiano wa serikali, wadau wa maendeleo na jamii kulinda mazingira ya bahari na rasilimali za uvuvi wakati wa warsha ya ujumuishwaji masuala ya bioanuwai katika usimamizi wa uvuvi inayoendelea  hoteli ya Giraffe Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 7 hadi 9, 2025.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Mhina (Kulia) na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uvuvi Nchini ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Uvuvi Bw. Chritian Nzowa wakifuatilia uwasilishwaji wa mada mbalimbali kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya bioanuwai katika usimamizi wa uvuvi wakati wa warsha inayoendelea hoteli ya Giraffe Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 7 hadi 9, 2025.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uvuvi Nchini ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Uvuvi Bw. Christian Nzowa akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Dkt. Charles Mhina kwenye warsha ya ujumuishaji masuala ya bioanuwai katika  usimamizi wa uvuvi, warsha inayofanyika Hoteli ya Giraffe Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 7 hadi 9, 2025.

Afisa Uvuvi Mkuu Bw. Owen Kibona akiwasilisha mapendekezo ya mpango mkakati wa ujumuishwaji masuala ya bioanuwai katika usimamizi wa sekta ya uvuvi wakati wa warsha inayoendelea katika hoteli ya Giraffe Jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 7 hadi 9, 2025.

Katibu wa Mtandao wa Wanawake Wavuvi na Wachakataji wa Mazao ya Uvuvi (TAWFA) Bi. Hadija Malibiche akieleza jinsi umoja huo unavyounga jitihada za kulinda bioanuwai katika uvuvi wakati wa warsha hiyo inayifanyika Hoteli ya Giraffe jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 7 hadi 9, 2025.

Wataalam wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wadau wa sekta ya uvuvi wakiwa katika majadiliano ya kuandaa mpango kazi wa ujumuishwaji wa masuala ya bioanuwai katika Sekta ya uvuvi wakati wa warsha inayofanyika Hoteli ya Giraffe Jijini Dar es Salaam kuanzia oktoba 7 hadi 9, 2025.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni