BI. MEENA AHIMIZA USHIRIKIANO KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI
Na. Stanley Brayton Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena amewataka Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwa na Ushirikiano katika utekelezaji majukumu Wizarani hapo. Bi. Meena amesema hayo Juni 28, 2025 wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Nyaraka za Ofisi baina yake na Mtangulizi wake Prof. Riziki Shemdoe katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya wizara hiyo yaliyopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma. Aidha Bi. Meena amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumteua katika nafasi hiyo ambapo ameahid kutekeleza maelekezo yote aliyopewa wakati akiapishwa. Kwa upande wake aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe, amewashukuru Watumishi wote wa Wizara hiyo, kwa ushirikiano alioupata na kazi kubwa waliyoifanya katika kipindi chake. Vilevile, Prof. Shemdoe amewasihi Watumishi wote kuishi kama familia, kuombeana mema na kuheshimiana ikiwa ni pamoja na ku...