Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Mhe. Abdallah Ulega na Waziri wa Kilimo, Maliasili, na Mifugo wa Jamhuri ya
Rwanda, Mhe. James Kabarebe wamesaini hati ya makubaliano ya kushirikiana
kuendeleza tasnia ya maziwa baina ya nchi hizo mbili.
Tukio hilo la utiaji saini
limefanyika Visiwani Zanzibar Januari
12, 2024 sambamba na Sherehe za Kutimiza Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar.
Akizungumza katika tukio
hilo, Waziri Ulega alisema kuwa ushirikiano huo ambao umekusudia kuendeleza
viwanda vya usindikaji wa maziwa utasaidia kuongeza uzalishaji wa maziwa wa
nchi hizo mbili jambo ambalo litapelekea kupatikana kwa ajira, usalama wa
chakula na kukuza uchumi wa kaya na mtu mmoja mmoja kupitia mnyororo wa thamani
wa maziwa.
Alisema kuwa mpaka sasa
bado nchi inaagiza maziwa mengi kutoka nje ya nchi, lakini kupitia ushirikiano
huo ana uhakika uzalishaji wa maziwa nchini utaongezeka na kuchechemua biashara
baina ya nchi hizo mbili. “Tanzania na Rwanda tumeamua kushirikiana katika
mambo mbalimbali ya Maendeleo ya Tasnia ya Maziwa, Niwahakikishie ndugu zangu
wa Rwanda na Tanzania kuwa nitawapa ushirikiano, nitasimamia utekelezaji wa
makubaliano haya tuweze kufikia malengo tuliyoyakusudia”, alisema Ulega
Aidha, Waziri Ulega
alimshukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kufungua milango
ya ushirikiano baina ya Tanzania na nchi nyingine akiongeza kuwa ushirikiano
huo ni moja ya hatua zake za kuhakikisha Watanzania wanaendelea kunufaika
kupitia rasilimali zao.
Kwa upande wake, Waziri wa
Kilimo, Maliasili, na Mifugo wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. James Kabarebe alisema
amefarijika na hatua hiyo iliyofikiwa kwani waliisubiri muda mrefu na ni imani
yake kuwa tija kubwa itapatikana katika tasnia hiyo ya maziwa kupitia ushirikiano
huo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega
(kulia) na Waziri wa Kilimo, Maliasili, na Mifugo wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe.
James Kabarebe wakisaini hati ya makubaliano ya kushirikiana kuendeleza tasnia
ya maziwa baina ya hizo katika hafla iliyofanyika Visiwani Zanzibar Januari 12, 2024 sambamba na Sherehe za
Kutimiza Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Mhe. Abdallah Ulega (kulia) na Waziri wa Kilimo, Maliasili, na Mifugo wa
Jamhuri ya Rwanda, Mhe. James Kabarebe wakipeana mikono punde baada ya kusaini
hati ya makubaliano ya kushirikiana kuendeleza tasnia ya maziwa baina ya nchi
hizo mbili katika hafla iliyofanyika Visiwani Zanzibar Januari 12, 2024 sambamba na Sherehe za
Kutimiza Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Mhe. Abdallah Ulega (wa tatu kutoka kushoto) na Waziri wa Kilimo, Maliasili, na
Mifugo wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. James Kabarebe (wa pili kutoka kushoto)
wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali punde baada ya tukio la
kusaini hati ya makubaliano ya kushirikiana kuendeleza tasnia ya maziwa baina
ya nchi hizo mbili katika hafla iliyofanyika Visiwani Zanzibar Januari 12, 2024 sambamba na Sherehe za
Kutimiza Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Wa nne kutoka kulia ni
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January
Makamba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni