DKT KIJAJI AIAGIZA NARCO KUZALISHA MBEGU ZA MIFUGO, MALISHO KWA WINGI
Na. Stanley Brayton ◼️Ataka visima 6 vya maji NARCO kukamilishwa Kabla ya January 5, 2025 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameiagiza Kampuni ya Ranchi za Taifa NARCO iliyopo Kongwa Jijini Dodoma Kuongeza wigo wa Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mifugo na Malisho itakayoongeza upatikanaji wa Nyama nchini na Kukuza uchumi wa Wafugaji. Dkt. Kijaji ametoa maagizo hayo Leo Desemba 17, 2024 Wakati wa Ziara yake kwenye Kambuni ya Ranchi za Taifa NARCO na kuahidi kurudi Januari 5, 2025 ili kuona utekelezaji wa maagizo hayo. " NARCO Mnajukumu la kuzalisha mbegu bora za aina Mbalimbali, Watanzania wanahitaji mifugo inayouzika kwa urahisi hapa ndani ya nchi na Kimataifa tunataka kila mfugaji akiuza Ng'ombe apate Milioni Nne hivyo nawataka Mzalishe mbegu Bora kwaajili wafugaji wetu" amesema Dkt. Kijaji. Kuhusu uzalishaji wa Mbegu za Malisho Dkt Kijaji amemwagiza Mkurugenzi wa Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko Stephen Michael kushirik...