Nav bar

Alhamisi, 31 Agosti 2023

WAZIRI ULEGA ANADI FURSA ZA AJIRA SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI KWA WAKUU WA MIKOA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amewahimiza Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala kuwahamasisha wananchi kuchangamkia fursa zilizopo kwenye sekta za mifugo na uvuvi ili waweze kujiongezea kipato na kujikwamua kimaisha.


Waziri Ulega aliyasema hayo muda mfupi baada ya kutoa mada kuhusu fursa za ajira zinazopatikana kwenye sekta za mifugo na Uvuvi wakati wa mafunzo ya uongozi kwa Viongozi hao yanayoendelea kufanyika kwenye shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha, Mkoani Pwani Agosti 26, 2023.

"Naomba nitumie fursa hii kuwashawishi hata nyinyi Viongozi kuingia katika fursa hizi hususan za ufugaji wa ng'ombe, kwani zina manufaa makubwa sana, kwa mfano ukianza kufanya unenepeshaji wa ng'ombe nakuhakikishia huwezi kuacha kwa jinsi ilivyo nzuri", alisema


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya hoja zilizoibuliwa na  Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala muda mfupi baada ya kutoa mada kuhusu fursa za ajira zinazopatikana kwenye sekta ya mifugo na Uvuvi wakati wa mafunzo ya uongozi kwa Viongozi hao yanayoendelea kufanyika kwenye shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha, Mkoani Pwani Agosti 26, 2023. Katikati ni Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ORTAMISEMI) Mhe. Angellah Kairuki na wa kwanza kushoto ni Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiwasilisha mada kwa  Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala kuhusu fursa za ajira zinazopatikana kwenye sekta ya mifugo na uvuvi wakati wa mafunzo ya uongozi kwa Viongozi hao yanayoendelea kufanyika kwenye shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha, Mkoani Pwani Agosti 26, 2023.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiongea na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala muda mfupi baada ya kutoa mada kuhusu fursa za ajira zinazopatikana kwenye sekta ya mifugo na Uvuvi wakati wa mafunzo ya uongozi kwa Viongozi hao yanayoendelea kufanyika kwenye shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha, Mkoani Pwani Agosti 26, 2023.


Sehemu ya Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (hayupo pichani) wakati  alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu fursa za ajira zinazopatikana kwenye sekta ya mifugo na Uvuvi wakati wa mafunzo ya uongozi kwa Viongozi hao yanayoendelea kufanyika kwenye shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha, Mkoani Pwani Agosti 26, 2023.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni