Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2022

SERIKALI YATAMBUA MCHANGO WA WANAWAKE SEKTA YA UVUVI

Picha
Serikali imesema wanawake wamekuwa na mchango mkubwa katika kusimamia rasilimali za uvuvi na wamekuwa wadau wakubwa katika kuhakikisha kuwa, biashara ya mazao ya uvuvi inaimarika ndani na nje ya nchi. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia suala la udhibiti ubora wa Mazao ya uvuvi na masoko, Bw. Steven Lukanga kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah wakati akizindua mtandao wa wanawake, wanaojihusisha na Shughuli za Uvuvi Tanzania (TAWFA) Kanda ya Ziwa Tanganyika ambapo amewataka wanawake kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuwa na sauti moja itakayowasaidia katika kutatua changato mbalimbali, Julai 27,2022 Mkoani Kigoma. Alisema mchango huo wa wanawake unastahili kupewa thamani kubwa hasa katika kuweka mikakati ya kusimamia changamoto zao ikiwemo kuanzisha Dawati la Jinsia la Uvuvi Wizarani ili shughuli za masuala ya wanawake ziweze kuratibiwa. “ninatambua kuwa wanawake wamejiunga katika vikundi mbalimbali ambavyo vinarahisisha u...

​SERIKALI YATAMBUA MCHANGO WA WANAWAKE SEKTA YA UVUVI

Picha
  Serikali imesema wanawake wamekuwa na mchango mkubwa katika kusimamia rasilimali za uvuvi na wamekuwa wadau wakubwa katika kuhakikisha kuwa, biashara ya mazao ya uvuvi inaimarika ndani na nje ya nchi. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia suala la udhibiti ubora wa Mazao ya uvuvi na masoko, Bw. Steven Lukanga kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah wakati akizindua mtandao wa wanawake, wanaojihusisha na Shughuli za Uvuvi Tanzania (TAWFA) Kanda ya Ziwa Tanganyika ambapo amewataka wanawake kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuwa na sauti moja itakayowasaidia katika kutatua changato mbalimbali, Julai 27,2022 Mkoani Kigoma. Alisema mchango huo wa wanawake unastahili kupewa thamani kubwa hasa katika kuweka mikakati ya kusimamia changamoto zao ikiwemo kuanzisha Dawati la Jinsia la Uvuvi Wizarani ili shughuli za masuala ya wanawake ziweze kuratibiwa. “ninatambua kuwa wanawake wamejiunga katika vikundi mbalimbali ambavyo vinarahisisha...

​HOMA YA MGUNDA ISIWE KIKWAZO CHA KUTOKULA NYAMA

Picha
Na. Edward Kondela Serikali imesema ugonjwa wa Homa ya Mgunda usiwe kikwazo cha watanzania kutokula nyama na kwamba asilimia tisini ya nyama inayopitia kwenye machinjio rasmi iko salama. Akizungumza jijini Dodoma (27.07.2022) kupitia vyombo mbalimbali vya habari, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Hezron Nonga amesema, nyama ya mnyama anayechinjwa kwenye machinjio rasmi huwa inakaguliwa na mtaalamu wa mifugo wa serikali kabla ya kwenda sokoni ili kuepusha madhara yoyote kwa binadamu. Prof. Nonga amebainisha kuwa kutokana na utafiti uliofanywa umebaini kuwa mnyama ambaye ameathirika na vimelea vya ugonjwa wa Homa ya Mgunda akitolea mfano wa ng’ombe, nyama yake inakuwa na rangi ya njano hivyo ni rahisi kwa mtaalam wa mifugo kubaini nyama hiyo machinjioni na kutoruhusu kupelekwa sokoni. “Kuchinja mifugo kwenye machinjio na nyama ikaguliwe na daktari au mtaalamu wa mifugo wa serikali kwa kuwa tushaona ng’ombe akipata shida ya Homa ya Mgunda, nyama yake in...

SAUDI ARABIA YAKUSUDIA KUWEKEZA KWENYE RANCHI YA RUVU

Picha
Nchi ya Saudi Arabia kupitia  kampuni binafsi ya Kilimo ya “Crown” iliyopo nchini humo inakusudia kuwekeza kwenye ranchi ya Ruvu iliyopo mkoani Pwani ikiwa ni hatua ya awali kabla ya kujenga miundombinu ya kusindika mazao ya mifugo nchini. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao baina yake na Mkurugenzi Mtedaji  wa Kampuni hiyo Bw. Mohammad Iftikhar kilichofanyika leo (27.07.2022) kwenye Ofisi za Wizara hiyo zilizopo jijini Dar-es-salaam. Mhe. Ndaki amebainisha kuwa ujio wa wawekezaji hao unatokana na uboreshwaji wa shughuli za ufugaji unaoendelea nchini ambao kwa kiasi kikubwa umechochea ongezeko la uzalishaji wa mazao ya nyama, maziwa na ngozi. “Nimewaeleza wakutane na kampuni yetu ya ranchi za Taifa (NARCO) na leo mchana watakutana Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo na Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni hiyo ili waweze kuzungumza kwa undani kwa sababu fursa za uwekezaji kwenye ranchi zetu za taifa ni nyingi na...

TAFITI KUBORESHA MAENDELEO YA SEKTA YA UVUVI

Picha
Tafiti zinazofanywa kwenye sekta ya uvuvi zinalenga kuhakikisha wadau wa sekta hiyo wanaboresha shughuli zao katika mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi.   Hayo yamesemwa leo (25.07.2022) na mwakilishi wa Katibu Mkuu Sekta ya Uvuvi, Bw. Emmanuel Kayuni ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa sekta hiyo wakati akifungua mafunzo ya kuandaa vijarida sera yaliyofanyika kwenye ukumbi wa TAFORI Manispaa ya Morogoro.   Bw. Kayuni amesema kuwa tafiti zinazofanyika ni lazima matokeo yake yawafikie walengwa ambao ni wadau wa sekta ya uvuvi ili kuweza kuwanufaisha na kuboresha shughuli wanazozifanya katika mnyororo wa thamani wa sekta hiyo.   “Tafiti zinazofanyika ni lazima ziwafikie walengwa, kuzielewa na kuwasaidia kubalidilisha maisha yao katika shughuli wanazozifanyi, hapo tafiti hizo zinakuwa na tija katika kuleta maendeleo ya wadau wa sekta ya uvuvi na taifa kwa ujumla.” alisema Bw. Kayuni   Sekta ya Uvuvi imepanga kuzitumia tafiti zinaz...

VIFARANGA VYA KUKU KUTOKA NJE YA NCHI MWISHO JULAI 30

Picha
Na. Edward Kondela   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema baada ya tarehe 30 mwezi huu, hakuna vifaranga vya kuku vitakavyoingizwa hapa nchini na kwamba serikali haitoi tena vibali vya kuingiza vifaranga hivyo.   Naibu Waziri Ulega amebainisha hayo (22.07.2022) jijini Dodoma wakati wa kikao cha wizara na wadau wa tasnia ya kuku, kujadili namna ya kukuza tasnia hiyo ambapo lengo la hatua hiyo ni utekelezaji wa sheria ya mwaka 2006 ambapo serikali imekuwa ikizuia uingizaji wa vifaranga nchini kutoka nje ya nchi ili kudhibiti ugonjwa wa mafua ya ndege kwa mifugo jamii ya ndege na kulinda wazalishaji wa kuku ndani ya nchi. Akizungumza wakati akifunga kikao hicho kilichojadili ajenda mbalimbali zikiwemo za upatikanaji wa vifaranga vya kuku, chakula cha kuku na bei ya kuku sokoni, Mhe. Ulega amesema ni mategemeo kuwa serikali haitaona vifaranga vinaingizwa nchini kutoka nje ya nchi na kutaka kuwepo kwa mfumo wa taarifa zinazohusu wazalishaji wa vifaranga...

WATAFITI WATAKIWA KUSAIDIA SEKTA YA MIFUGO

Picha
Na Mbaraka Kambona,  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amewataka Watafiti wa Mifugo nchini kuhakikisha wanafanya tafiti zitakazosaidia Sekta ya Mifugo kuzalisha kwa tija na kuwa na mchango mkubwa katika pato la taifa. Waziri Ndaki alitoa wito huo wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Mifugo uliofanyika jijini Dodoma Julai 21, 2022. Akiongea na wadau hao, Waziri Ndaki alisema wafugaji wengi nchini bado wanafuga kienyeji  na kupelekea sekta ya mifugo kutokuwa na tija kubwa, hivyo ni wakati sasa watafiti wasaidie kutatua changamoto hiyo.  "Kama tutaendelea kufuga kama tunavyofuga leo kwa kuswaga Ng'ombe, baada ya miaka kumi ijayo tutaleta shida kwenye nchi hii, kwa sababu maeneo ya malisho yamepungua, hivyo watafiti watusaidie kuja na majibu yanayolenga kutatua changamoto hii, tuone namna gani tutakabiliana na jambo hili", alisema Aliongeza kwa kusema kuwa kwa upande wa Wizara kuanzia mwaka huu wa fedha  wamejipanga kufanya kampeni kubwa ya kuwaelim...

WAFUGAJI KUELIMISHWA UFUGAJI WA TIJA NA KIBIASHARA, KUONDOKANA NA UMASIKINI

Picha
Edward Kondela Serikali imesema lengo kubwa la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa wafugaji ni kukuza tija na kuwasaidia kufuga kibiashara ili waweze kunufaika kupitia mifugo yao.   Akizungumza (15.07.2022) wakati akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwenye maonesho ya mifugo na mnada yanayofanyika katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani katika Shamba la mifugo la Mbogo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amesema shughuli za ufugaji na uvuvi zimekuwa zikiendeshwa kiasili hivyo kushindwa kukua na kubadili maisha ya wadau wa sekta hizo.   Waziri Ndaki amebainisha kuwa imani mbalimbali pia zimekuwa zikitawala kwa wafugaji na wavuvi kwenye shughuli zao na kusababisha kutopokea kwa haraka mabadiliko na kufanya shughuli hizo bila kufuata utaalamu, ujuzi, weledi na kufahamu hitaji la soko ili kufuga kwa tija na kibiashara.   “Tumeanza ngazi ya wizara kuzungumza juu ya tija zaidi na biashara zaidi kubadilisha mtazamo wa...

WAZIRI NDAKI AAGIZA BODI YA USHAURI KUJIKITA KWENYE URASIMISHAJI SEKTA YA MAZIWA

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amewataka wajumbe wa bodi ya ushauri ya Bodi ya Maziwa Tanzania kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya maziwa nchini ikiwemo kurasimisha sekta hiyo kwa kasi na kuweka vituo ambavyo vitakusanya maziwa Kwa pamoja ili kuondokana na masoko yasiyo rasmi na kusaidia  kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini.   Mheshimiwa Ndaki amezungumza hayo jijini Dodoma leo Julai 14, 2022 wakati akifanya uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Bodi ya Maziwa Tanzania ambapo amesema kuwa uzalishaji wa maziwa nchini upo chini ambapo kwa sasa wastani wa lita bilioni 3.4 ndizo zinazozalishwa huku kiwango cha unywaji wa maziwa kikiwa ni lita 62 tu kwa mwaka kwa Mtanzania mmoja.   Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Maziwa nchini Dkt . George Msalya amebainisha mafanikio ya Bodi hiyo mpaka hivi sasa ikiwa ni pamoja na kukua kwa sekta ya maziwa nchini mpaka kufikia asilimia 2.3, kuratibu vituo 238 vya kukusanyia maziwa.   "Sekta yetu inakua kwa...