Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Mhe. Mashimba Ndaki (Mb) (wa tatu kutoka kushoto) na ujumbe kutoka Tanzania
wakiwa kwenye kikao kifupi na wenyeji wao wa Misri mara baada ya kuwasili Nchini humo lengo
likiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu na kukuza ushirikiano katika Sekta ya
Uvuvi. Februari 21, 2022.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Mhe. Mashimba Ndaki (wa pili kutoka kushoto) pamoja na ujumbe wake kutoka
Tanzania walitembelea Ofisi za National Service Projects Organization ya
Misri na kufanya mazungumzo na ujumbe
kutoka Misri ukiongozwa na Naibu Waziri wa Ulinzi Jenerali Medhat El Nahas, lengo likiwa ni pamoja na kueleza
fursa za ushirikiano na uwekezaji zilizopo katika Sekta ya Uvuvi Nchini
Tanzania. Februari 21,2022
Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Mhe. Mashimba Ndaki (Mb) (kushoto meza kuu ) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Taifa ya
Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji Misri, Jenerali Eslam Attia Rayan, wakiwa na ujumbe kutoka Tanzania na ujumbe kutoka Misri
wakati wa ziara rasmi nchini humo, lengo
likiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu na kukuza ushirikiano katika Sekta ya
Uvuvi. Februari 21, 2022.
Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto waliokaa) na Mwenyekiti
wa Bodi ya Kampuni ya Taifa ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji Misri Jenerali Eslam Attia Rayan wakitia saini
kwenye hati ya makubaliano ya
ushirikiano Kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) na Kampuni ya Taifa ya
NCFA. Februari 21, 2022 nchini Misri, lengo likiwa ni kukuza ushirikiano na
uwekezaji katika minyororo ya thamani ya uvuvi na ukuzaji viumbe maji pamoja na
kukuza utaalam katika Sekta ya Uvuvi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni