Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki ametoa maelekezo manne kwa wataalam wa mifugo wanaohusika na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kwa lengo la kuhakikisha wanafikia lengo lililowekwa.
Waziri
Ndaki ametoa maelekezo hayo leo (20.01.2022) kwenye kikao na wataalam hao
kilichofanyika kwenye ukumbi wa Royal Village ambapo aliwaeleza kuwa mwenendo
wa ukusanyaji wa maduhuli ya serikali sio mzuri kwani kati ya bilioni 50
zilizokusudiwa kukusanywa ni bilioni 13.9 ndio zimekusanywa.
Katika
kikao hicho taarifa za ukusanyaji wa maduhuli ya serikali ziliwasilishwa kwa
kila kituo ambapo pia changamoto ziliwasilishwa na kujadiliwa namna gani ya
kuweza kukabiliana nazo ili kuhakikisha ukusanyaji wa maduhili unafikia malengo
yaliyowekwa
Akizungumza
na wataalam hao Waziri Ndaki amesema kuwa wizara iliamua kuunda timu ya
ufuatiliaji kwa lengo la kuangalia hali ya ukusanyaji wa maduhuli ya serikali
kwenye minada na vituo vilivyo chini ya wizara. Timu hiyo ilibaini changamoto
mbalimbali na kutoa mapendekezo ambayo yatasaidia kuongeza ukusanyaji wa
mapato.
Baada
ya majadiliano ya taarifa zilizokuwa zimewasilishwa, Waziri Ndaki aliwaeleza
wataalamu hao kuwa ni lazima wajipange vizuri kuhakikisha wanafikia malengo ya
ukusanyaji maduhuli ya serikali kama walivyo pangiwa.
"Viongozi
tutaendelea kuwafuatilia kwa karibu ili kuhakikisha malengo ya ukusanyaji
maduhuli ya serikali yanatimizwa na kwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu
kwa makusudi hatua zitachukuliwa dhidi yake," alisema Waziri NDAKI
Pia
amemueleza Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayesimamia sekta ya Mifugo,
Bw. Tixon Nzunda kuwasiliana na Katibu Mkuu TAMISEMI ili kuhakikisha
Halmashauri zilizotumia fedha za makusanyo ya maduhuli za wizara zikiweno za Halmashauri
Mvomero, Tarime na Manyoni zinarejesha fedha hizo.
Lakini
pia wataalam wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na kwa kujitolea
ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa ya ukusanyaji wa maduhuli ya serikali
yanatimizwa. Waziri Ndaki amewaeleza wataalam hao kuwa katika muda wao wa
utumishi ndani ya sekta ya mifugo ni lazima waache alama ikiwemo ya ukusanyaji
mzuri wa maduhuli. Wataalam hao wametakiwa kuwa wabunifu katika ukusanyaji wa
maduhuli ya serikali na kuhakikisha wanasimamia sheria, kanuni, miongozo na
taatibu zilizowekwa.
Naye
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayesimamia Sekta ya Mifugo, Bw. Tixon
Nzunda amewataka wataalam hao kwenda kufanya kazi kwa uadilifu lakini pia
watalazimika kuwajibika kutokana na matendo yao kwenye suala la ukusanyaji wa
mapato. Vilevile amewataka kuhakikisha wanakusanya mapato katika maeneo yao na
kucha tabia ya udanganyifu kwani hatua zitachukuliwa dhidi yao. Adiha, amewataka
wataalam hao kuwasilisha taarifa za makusanyo kila mwezi.
Pia
amemshukuru Waziri kwa uamuzi wake wa kuitisha kikao hicho kwani kimesaidia kwa
kuwawezesha wataalam wanaohusika na ukusanyaji wa maduhuli Tanzania Bara kukaa
kwa pamoja kujadili changamoto walizonazo na kutoka na mkakati wa pamoja ili
kuhakikisha ukusanyaji wa maduhuli unakwenda vizuri.
Mkuu
wa Mnada wa Ipuli mkoani Tabora, Fred Senyagwa amesema kuwa watakwenda
kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Waziri ili kuhakikisha wanakusanya maduhuli
kulingana na malengo yaliyowekwa.
Kaimu
Mkuu wa Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo - Iringa, Bw. Rajon Deule
amesema kuwa sababu ya kituo chao kufanya vizuri ni kwamba Kanda yao wamekuwa
wakifanya vikao vya mara kwa mara ambavyo huwa wanajadili changamoto
wanazokutana nazo na kujiwekea mikakati ya namna ya kukabiliana nazo. Kwa
kutumia njia hiyo imewasaidia kuweza kukusanya maduhuli ya serikali vizuri.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma
za Mifugo, Prof. Hezron Nonga akitoa ufafanuzi wakati wa kikao cha Waziri na
Wataalam wa Mifugo wanaohusika na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali
kilichofanyika kwenye ukumbi wa Royal Village Jijini Dodoma. (20.01.2022)
Baadhi ya Viongozi na Wataalam wa Sekta ya Mifugo wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa kuhusu ukusanyaji wa maduhuli kwenye sekta hiyo wakati wa kikao cha Waziri wa Mifugo nna Uvuvi na Wataalam wa Mifugo wanaohusika na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kilichofanyika kwenye ukumbi wa Royal Village Jijini Dodoma. (20.01.2022)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni