Wafugaji Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani wawezeshwa na Serikali madume matatu ya ng'ombe aina ya borani ikiwa ni pamoja na kuwakwamua wafugaji hao kiuchumi.
Wakati akikabidhi madume hayo Januari 27. 2022, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega alisema madume hayo matatu ya ng`ombe aina ya borani yatakwenda kuboresha koosafu za ng`ombe wa asili kwa wafugaji watakao yatumia.
"ugawaji wa madume haya bora ya ng'ombe ni kwa lengo la kuboresha kosaafu za Mifugo Ili waelekee kwenye ufugaji wa kisasa na hii inaenda sambamba na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM (2020 – 2025) inayolenga kuwakwamua kiuchumi wafugaji nchini.
Naye Mkurugenzi wa ranch ya Mbogo, Chalinze Mkoani Pwani, Naweed Mulla ambaye wameshirikiana na Serikali kugawa madume hayo alisema thamani ya madume ni shilingi milioni 15.
“Uzalishaji wa Ng’ombe hawa aina ya borani utasaidia kuboresha koosafu bora ambayo watakuwa bora kwenye uzalishaji wa mazao ya mifugo ikiwemo kiwango kikubwa cha maziwa, nyama nyingi, uhimilivu dhidi ya magonjwa na hali ya mazingira ya mikoa yetu” alisema Mulla
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri pia aligawa majokofu 8 kwa vikundi vya wanawake wajasiriamali kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya Uvuvi Ili kusaidia kupunguza upotevu wa ubora wa mazao hayo na kuongeza thamani.
Mratibu wa miradi ya Pwani ya bahari ya Hindi nchini kwa miradi inayotekelezwa na Shirika linalojishughulisha na mazingira (WWF), Dkt. Modesta Medadi alisema wamekabidhi majokofu 8 kwenye Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, ikiwa ni mkakati wa kuwezesha shughuli zao.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ally alimshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada yake ya kusaidia na kuwaendeleza wafugaji na wajasiriamali wa bidhaa za uvuvi nchini sawa na ahadi yake katika hotuba zake.
Naibu Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, akilishukuru Shirika linalojihusisha na
mazingira (WWF) kwa kuwawezesha kupata majokofu nane (8) kwenye Wilaya ya
Mkuranga na kuwasihi wanawake wajasiriamali waliokabidhiwa majokofu hayo
wayatunze na wayatumie kama ilivyokusudiwa. Januari 27.2022
Naibu Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiongea na wafugaji pamoja na vikundi vya
wanawake wa Mkuranga wakati wa hafla fupi wa ugawaji wa madume bora aina ya
borani na majokofu Januari 27, 2022.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni