Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2021

MIFUGO YA TANZANIA YAHITAJIKA VIETNAM NA WAZIRI NDAKI AWAALIKA WAVIETNAM KUFUGA SAMAKI

Picha
Na. Edward Kondela   Balozi wa Vietnam nchini Tanzania Mhe. Nguyen Nam Tien amesema atawasilisha serikalini vigezo vinavyopaswa kufuatwa na wafanyabishara wa hapa nchini ili waweze kusafirisha mifugo na nyama kwenda nchini Vietnam, kutokana na nchi hiyo kuwa na uhitaji mkubwa wa nyama.   Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amebainisha hayo leo (28.04.2021) ofisini kwake katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, mara baada ya kuwa na mazungumzo mafupi na balozi huyo aliyefika ofisini kwa Waziri Ndaki ili kuimarisha mahusiano baina ya Tanzania na Vietnam na kupeana uzoefu katika sekta za mifugo na uvuvi.   Mhe. Ndaki amesema Balozi Tien amesema nchi ya Vietnam ina uhitaji mkubwa wa nyama kwa kuwa wana ng’ombe wasiozidi Milioni Sita hivyo kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kuchangamkia fursa hiyo endapo watakidhi vigezo vya kusafirisha mifugo na nyama nchini humo.   “Tunaweza kutumia fursa hii kusafirsha ng’ombe au nyama na kwamba w...

UVUVI HARAMU KUDHUBITIWA BWAWA LA MUNGU

Picha
Serikali kwa kushirikiana na wadau imepanga kudhibiti Uvuvi haramu kwenye Bwawa la Nyumba ya Mungu lililopo Mkoani Kilimanjaro.   Haya yamesemwa na Katibu Mkuu anayesimamia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah leo (28.04.2021) baada ya kumalizika kwa kikao cha ujirani mwema kilichojadili kuhusu ulinzi na usimamizi wa rasilimali za Uvuvi kwenye Bwawa la Nyumba ya Mungu. Kikao hicho kiliwajumuisha Viongozi na Wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wilaya za Mwanga, Moshi na Simanjiro kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Kindoroko wilayani Mwanga.   Dkt. Tamatamah amesema kupitia kikao hicho wamejadili kwa kina kuhusu tatizo la Uvuvi haramu unaofanyika kwenye Bwawa la Nyumba ya Mungu na kutoka na maazimio ambayo Wizara na Halmashauri zilizoshiriki pamoja na wadau watakwenda kuyasimamia utekelezaji wake lengo likiwa ni kudhibiti shughuli za uvuvi haramu katika bwawa hilo. Moja ya maazimio hayo ni pamoja na udhibiti wa uuzwaji wa samaki wadogo kwenye masoko yana...

SERIKALI YAMALIZA MGOGORO WA ARDHI BAINA YA WANANCHI NA NARCO

Picha
Na Mbaraka Kambona, Kigoma   Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ameielekeza Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kutenga Ekari Elfu Kumi na Tano (15000) na wazigawe kwa Wananchi wa Vijiji viwili vya Mpeta na Chakulu vilivyopo Wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma ili kutatua mgogoro wa ardhi wa muda mrefu baina ya wananchi hao na Kampuni hiyo.   Ndaki alitoa maelekezo hayo Aprili 25, 2021 katika ziara yake Wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma kwa lengo kutatua mgogoro huo wa ardhi kufuatia wananchi wa vijiji hivyo kuvamia maeneo ya Ranchi ya Uvinza na kuishi humo kinyume na taratibu.   Akiongea na wananchi wa vijiji hivyo kwa nyakati tofauti, Waziri Ndaki alisema kuwa Serikali imeamua kufikia maamuzi hayo ili wananchi hao waweze kujikita katika shughuli za maendeleo na kuachana na migogoro ya kila siku ambayo haina tija yoyote.   “Hatupendi tuendelee na migogoro kwenye maeneo yetu, tunataka tumalize migogoro ili tuanze kufanya shughuli za maendeleo, kila mwan...

ULEGA ATAKA KUCHANGAMKIWA KWA SOKO LA KAA NA JONGOO BAHARI!

Picha
Na. Edward Kondela   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amewataka wananchi wanaofanya shughuli zao katika Ukanda wa Bahari ya Hindi kuchangamkia fursa ya ufugaji viumbe maji wakiwemo kaa na jongoo bahari ambao wamekuwa na soko kubwa nje ya nchi.   Akizungumza mwishoni mwa wiki (24.04.2021) katika Kijiji cha Tawalani kilichopo kata ya Manza iliyopo Wilaya ya Mkinga, Mkoani Tanga, wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani humo, Mhe. Ulega amesema Ukanda wa Bahari ya Hindi bado haujatumiwa vyema katika kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, hivyo wananchi kujikita zaidi katika uvuvi na kutojishughulisha na ufugaji wa viumbe maji ambao wamekuwa wakitakiwa nchi mbalimbali.   Mhe. Ulega amebainisha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekuwa akizungumzia sana Sekta ya Uvuvi kuwekeza kwenye uchumi wa bluu, hivyo wananchi hususan wanaofanya shughuli za uvuvi wanatakiwa kuongeza wigo wa shughuli...

ULEGA - “MKIRUHUSU MIFUGO IPITE NJIA ZA PANYA NCHI ITAKOSA MAPATO”

Picha
Na. Edward Kondela   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amewataka wananchi wa Kijiji cha Horohoro Kijijini Kata ya Duga katika Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, kutoruhusu mifugo ipitishwe kinyemela mpakani kwenda nchi jirani badala yake wawafichue wanaofanya hivyo ili kuwadhibiti kwani serikali inakosa mapato.   Mhe. Ulega aliyasema hayo mwishoni mwa wiki (24.04.2021) wakati alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo kwa kutembelea eneo lenye ekari 23 ambapo kutajengwa mnada wa mifugo kijijini hapo na kusema kuwa mnada huo utakuwa chachu ya kuinua maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.   Alisema lazima wananchi wilayani hapo kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri wa kudhibiti mifugo kupitishwa kinyemela kwenda nje ya nchi ili kuiwezesha serikali kukusanya mapato hatua ambayo itakuwa ni chachu kubwa kwao kuwezesha maendeleo.   “Niwaambie tu kwamba lazima hivi sasa tujipange kwa ujio wa fursa za mnada huu kwani baada ya miaka miwili eneo ...

SERIKALI KUJA NA MKAKATI ENDELEVU KUDHIBITI UVUVI HARAMU

Picha
Na Mbaraka Kambona, Kigoma   Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ipo katika mpango wa kuwa na mkakati endelevu wa kudhibiti uvuvi haramu na kuachana na utaratibu wa kuendesha oparesheni za muda mfupi.   Ndaki alisema hayo wakati akiongea na Wavuvi wanaofanya shughuli zao katika Mwalo wa Kibirizi ulipo katika Ziwa Tanganyika Mkoani Kigoma Aprili 24, 2021.   Akiongea na wavuvi hao Ndaki alisema kuwa lengo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi ni kuwa na udhibiti wa uvuvi haramu ambao utakuwa endelevu utakaoshirikisha wahusika wenyewe wanaofanya shughuli za uvuvi na viongozi wa eneo husika kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya hadi Mkoa.   “Tunataka kuja na mkakati endelevu wa namna ya kudhibiti uvuvi haramu, tuusike sote, kuanzia Wataalamu, Viongozi wa ngazi zote na wananchi wanaohusika na uvuvi wenyewe,” alisema Ndaki huku akiongeza kuwa   “Uvuvi haramu unatishia rasilimali zetu za uvuvi, tusiulee, tuwashirikis...