NDAKI: TUTABORESHA SEKTA YA MIFUGO KWA KUJENGA MAJOSHO 129
SERIKALI imesema kuwa katika mwaka wa fedha 2021/22 imepanga kuboresha sekta ya mifungo ikiwa ni pamoja na kujenga majosho 129, ili kuongeza thamani ya bidhaa zitokanazo na mazao ya mifugo. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki, aliyasema hayo jana jijini Dodoma, wakati wizara yake ilipokuwa kiwasilisha bajeti ya sekta ya mifugo kwenye kamati ya kudumu ya bunge ya kilimo, mifugo na maji. Alisema, Wizara hiyo imezamilia kufanya maboresho makubwa katika sekta ya mifugo ili kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na mifugo na kuchangia katika pato la taifa. Ndaki, alisema moja katika eneo ambalo watalifanyia kazi ni kujenga majosho 129, mapya pamoja na kukarabati yaliyopo ili kusaidia wafugaji kupata huduma hizo katika maeneo yao, “Tutahakikisha kuwa tunajenga majosho kwa ajili ya kuogeshea mifugo kila eneo lenye mifugo nchini lakini pia kukarabati majosho yote yalipo ili kuwezesha wafugaji kupata huduma za ugani katika maeneo yao”alisema Alisema, ...