Nav bar

Ijumaa, 29 Novemba 2019

HABARI PICHA NA MATUKIO

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akifanya tathmini ya ubora wa samaki aina ya jodari katika Soko la Samaki la Msasani jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mvuvi Duniani inayoaadhimisha Novemba 21 kila mwaka.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akikagua mwalo wa Soko la Samaki la Msasani jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili katika soko hilo kama mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Mvuvi Duniani inayoadhimishwa Novemba 21 kila mwaka.

Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji Dkt. Nazael Madala akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah wakati akizungumza na baadhi ya washiriki wakiwemo wavuvi kwenye maadhimisho ya Siku ya Mvuvi Duniani yaliyofanyika katika Soko la Samaki Msasani jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Mvuvi Duniani yaliyofanyika katika Soko la Samaki la Msasani jijini Dar es Salaam akizungumza na washiriki kwenye maadhimisho hayo ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza ufugaji samaki katika Ukanda wa Pwani, pamoja na kutoa zawadi kwa wavuvi walioshinda katika zoezi la uvuaji wa samaki aina ya jodari.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na baadhi ya washiriki wakiwemo wavuvi kwenye maadhimisho ya Siku ya Mvuvi Duniani yaliyofanyika katika Soko la Samaki la Msasani jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yanafanyika Novemba 21 kila mwaka.


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamin Sitta (Kulia) na Katibu Mtendaji wa Muungano wa Taifa wa Uvuvi wa Jodari Tanzania Bw. Winfried Haule wakizungumza na washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Mvuvi Duniani (hawapo pichani) yanayoadhimishwa Novema 21 kila mwaka, ambapo mwaka huu kitaifa yamefanyika katika Soko la Samaki la Msasani jijini Dar es Salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni