Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega yuko nchini Ethiopia ambapo anahudhuria mkutano wa
mawaziri wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wanaohusika na Kilimo,
mifugo, uvuvi, mazingira, maji na Maendeleo Vijijini.
Mkutano huo ulioitishwa na
Kamisheni ya Afrika kupitia Shirika lake la kusimamia Maendeleo ya Rasilimali
za Wanyama Barani Afrika (AU-IBAR), unafanyika kwa siku mbili mjini Addis Ababa
ambapo mbali na mambo mengine mkutano huo utapokea ripoti na maazimio
mbalimbali kutoka kwa wataalam wa sekta hizo kujadili na kuyapitisha ili waweze
kupeleka Halmadhauri Kuu ya AU kwa maamuzi na utekezaji.
Moja ya mikakati, ripoti na
maazimio na mapendekezo yanayotarajiwa kujadiliwa na kuridhiwa na baraza hilo
la mawaziri wa AU wa sekta ya mifugo, uvuvi, kilimo, mazingira na maji ni;
1. Ripoti ya miaka miwili
ya Tathmni ya Azimio la Malabo (Malabo Declaration) lenye lengo la kuondoa njaa
katika bara ka Afrika ifikapo Mwaka 2025.
2. Ripoti ya Tathnimi ya
kuwasiliana na Majanga ya asili kama mafuriko na ukame.
3. Ripoti ya hali ya hewa
na mabadiliko ya tabia nchi.
4. Juhudi za nchi wanachama
kuzuia matumizi ya bidhaa za plastiki.
5. Mkakati wa kupanda mazao
yenye viini lishe vya kutosha.
6. Mkakati wa kukabiliana
na upotevu wa mazao ya mimea na samaki baada ya kufunga (Post harvest Loss)
7. Mkakati wa kupambana na
magonjwa na vimelea sugu kwa mifugo.
8. Mpango wa kuanzisha
maabara za kupima ubora wa chakula katika bara la Afrika.
9. Mpango wa pamoja wa kuwa
na kusimamia na kuweza katika wazo la uchumi wa bahari (Blue economy).
10. Mpango mkakati wa miaka
10 kuendeleza uvuvi mdogo mdogo (small scale fisheries)
11. Mpango mkakati wa miaka
10 wa kuendeleza sekta ya ukuzaji viumbe maji.
Mkutano huo ulifunguliwa na
Mheshimiwa balozi Bi. Josefa Correia Sacko-mkuu wa Kamisheni ya Afrika ya
Kilimo na maendeleo vijijini, ambapo zaidi ya washiriki 300 kutoka nchi 49 za
bara la Afrika wanahudhuria wakiwepo wawakilishi wa mashirika ya kimataifa kama
FAO, WWF, Benki ya Dunia na NEPAD.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akifuatilia hoja mbalimbali katika kikao kinachoendelea Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni