TANZANIA YASHIRIKI KONGAMANO LA MATUMIZI ENDELEVU YA RASILIMALI ZA BAHARI NCHINI MSUMBIJI
Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi zikiwemo Tanzania, Kenya, Msumbiji na Afrika ya Kusini na Visiwa vya Ushelisheli zimepewa rai ya kuhakikisha zinafanya kila njia kulinda rasilimali za pamoja hususan zinazopakana na bahari ili ziweze kusaidia kukuza uchumi wa nchi hizo. Rai hiyo imetolewa na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakati wa ufunguzi wa kongamano la kujadili matumizi endelevu ya rasilimali za bahari linaloendelea katika mji wa Maputo nchini humo. Rais Nyusi amesema kongamano hilo la siku mbili lina umuhimu mkubwa kwa kuwa linafanyika wakati huu ambapo uvunaji holela na usiofuata utaratibu wa rasilimali za bahari umeshamiri katika nchi nyingi za bara la Afrika na Asia. Akihutubia washiriki wa Kongamano hilo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ameelezea hatua mbalimbali ambazo nchi ya Tanzania imepiga katika kuhakikisha malengo ya milenia kuhusu uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za asili yanafikiwa. Mhe. Ulega amezita...