Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imewezesha
kupatiwa hati miliki ya kimila Nne (4) kwa kikundi cha wafugaji cha Olengapa kupitia mradi wa Uendelezaji wa
Nyanda za Malisho (SRMP).
Tukio hilo la kukabidhi hati miliki ya kimila kwa Kikundi
cha Wafugaji lilifanyika katika Kijiji cha Lengatei Wilaya ya
Kiteto Mkoa wa Manyara.
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia mradi wa SRMP imeweza kutoa hati
hiyo kwa kikundi cha wafugaji cha Olengapa vinavyoruhusu kutumia na kumiliki
eneo la malisho kwa pamoja.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Sekta ya Mifugo,Prof
Elisante Ole Gabriel, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Zakariyya
Kera alisema, eneo hilo lililotengwa linaukubwa wa hekta 30,145.
Alisema pia, lengo ni kuwapatia haki wafugaji ya uhakika wa kumiliki Ardhi
kwa shughuli zao za kiuchumu na kijamii.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Bw. Manyara
Alexanda Mnyeti, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Bw. Tumaini Magesa alisema, nashukuru
wizara ya Mifugo na uvuvi kuheshimu ilani ya Chama cha mapinduzi kwasabau ni
hitaji la chama tawala na hili limefanikiwa.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bw. Zakariyya Kera akisoma hotuba kwa ufupi kwa niaba ya Katibu Mkuu sekta ya Mifugo. |
Mwenyekiti wa kikundi cha Olengapa Bw. Kilekeni Noongejeck akipokea hati miliki ya kimila kwa niaba ya kikundi kutoka kwa mgeni rasmi Bw. Tumaini Magesa |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni