SERIKALI IPIME MAENEO YA WAFUGAJI ILI WAMILIKISHWE KISHERIA
Wafugaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro wamewalalamikia watendaji wa Serikali na kwamba wao ndio wanao chochea Migogoro kati ya Wakulima na Wafugaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai. Malalamiko hayo yametolewa jana na wafugaji wa kijiji cha Sanya Station, katika kata ya Kia, katika Halmashauri ya Wilaya Hai, walipokuwa wakitoa kero zao kwa Katibu Mkuu Mifugo, Prof.Elisante Ole Gabriel, aliyefika katika kijiji hicho kusikiliza kero za wafugaji hao kwa Niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe .Luhaga Joelson Mpina. “Sisi Wafugaji na Wakulima natuna tatizo kabisa, Shida kubwa iko kwa hao Mgambo, ambao wanatumwa na watendaji wa Serikali waje wakamate Ngombe wetu bila kosa lolote na kufanya mradi wao wa kuwaingizia fedha;.alisikika Mfugaji akilalamika. Aidha watumishi waliopo katika taasisi za Umma za NARCO na TALIRI ,West Kilimanjaro nao wamelalamikiwa na wafugaji hao kuwa ni vinara wa kuchukua rushwa hasa Ngombe wa wafugaji wan...