Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Saame amewataka wataalamwa Sekta ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha wanachukua takwimu sahihi wakati wa kukusanyataarifa za kitafiti ili ziweze kuisaidia Serikali katika kupanga mipango yake. Waziri Shaame ameyasema hayo wakati akifunga Kongamano la 46 la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Mkutano Mkuu wa 47 wa Mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) lililofanyika kwenye Ukumbi wa Olasit Garden, Arusha Oktoba 27, 2023. "Takwimu sahihi kuhusu taarifa za mifugo na uvuvi zitasaidia kutunga sera, kunyoosha maono, fikra na miongozo ya ilani ya chama cha mapinduzi kuweza kufikia malengo ya kuwainua wananchi kupata mafanikio kwa haraka," alisema Aliongeza kwa kusema kuwa Serikali inawategemea sana wataam na hivyo watumie vizuri teknolojia walizonazo ili zikaboreshe tasnia nzima ya ufugaji ili kupata maendeleo. “Wizara ...
Na, Edward Kondela Serikali imeanza utekelezaji wa ufugaji samaki kwa njia ya vizimba katika Ziwa Tanganyika baada ya mpango huo kuonesha mafanikio makubwa katika Ziwa Victoria. Akizungumza (11.01.2024) katika Mwalo wa Kasanga uliopo Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti amesema tayari wizara imeanza kutoa elimu kwa wavuvi wa ukanda wa Ziwa Tanganyika kabla ya kufikisha vizimba hivyo na mbegu bora za samaki. Mhe.Mnyeti ameongeza kuwa kwa sasa serikali imetenga Shilingi Bilioni 20 kwa ajili uwekaji vizimba katika Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa sababu ufugaji wa samaki unakua kwa kasi maeneo mbalimbali duniani kutokana na upungufu wa samaki waliopo kwenye maji ya asili yakiwemo mabonde, maziwa, mito na bahari kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya uharibifu wa mazingira, ongezeko la watu na uharibifu wa mazalia ya samaki. Ameongeza kuwa ili kunusuru upungufu wa samaki katika masoko ya ndani na nje ya nchi serikali imeamua ...
TANZANIA DAIRY BOARD (TDB) Milk for Health and Wealth creation EMPLOYMENT OPPORTUNITY Tanzania Dairy Board (TDB) was established by the Dairy Industry Act Cap.262 of 2004 and is mandated to develop, regulate and promote the Dairy Industry in Tanzania mainland. The Board promotes production, collection, processing, marketing and consumption of quality milk and dairy products by facilitating stakeholders’ activities. In order to implements its objectives, TDB would like to invite suitably qualified Tanzanians to join its lean, entrepreneurial and dynamic team by filling the following vacancies: 1. Dairy Production Services Officer II– 1 Post i. Duty Station: Dar es Salaam ii. Reporting To: Dairy Technical Services Department Manager Dairy Production Services Officer will be responsible for advising the dairy stakeholders to ensure compliance to Dairy Industry Act and its regulation. She/he will be specifically responsible for dairy inspection, provision of advisory serv...
Maoni
Chapisha Maoni