TASFAM YAIWEZEASHA MAABARA YA TAIFA YA UVUVI NCHINI (DSM), KUISAKA ITHIBATI YA KIMATAIFA
Na. Edward Kondela
Maabara ya Taifa ya Uvuvi nchini (NFQCLAB), Kituo cha Dar es Salaam, kupitia Mradi wa Kukuza Usimamizi Endelevu wa Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji wa Bahari Tanzania (TASFAM), yafanya kikao maalum kupata miongozo 24 ya kuwezesha maabara hiyo kuwa na mfumo wa kimataifa ili kupata ithibati ya ISO/IEC 17025.
Kikao hicho kinafanyika Mjini Morogoro, ambapo baadhi ya wataalamu wanakutana kwa wiki moja kuanzia Tarehe 8 hadi 15 Aprilii 2026 kwa ajili ya kuandaa mfumo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kupata ithibati na kuifanya kuaminika kimataifa kwa kuthitibitisha ubora wa mazao ya uvuvi na kukubalika katika masoko ya kimataifa.
ISO/IEC 17025 ni Kiwango cha Kimataifa kinachotumika kwa maabara za upimaji (testing) na upimaji sahihi/ugezi (calibration) ili kuthibitisha kuwa maabara zinafanya uchunguzi na kutoa majibu sahihi yanayokubalika kimataifa, hivyo kuongeza imani kwa wadau na kurahisisha biashara ya kimataifa.




Maoni
Chapisha Maoni